Shibuda awashangaa wanaoogopa urais



mkuu
sasa chukulia watokee watu kama SAS,Mwandosya,Kigoda..au hata lowasa..watu wa type hiyo
halafu eti useme kikwete atapitishwa tu!!!
 

Halafu Malecela akasema ccm ni chama cha masikini,sasa hilo group hapo juu ndilo linalofanya maamuzi kwa niaba ya masikini wa ccm na Tanzania kwa ujumla....?Inashangaza sana.
 

Hakuwa tu anaongea pumba, bali pia alikuwa anawatukana watanzania, siku zote tumeona na kupima utendaji wa kazi wa CCM na Kikwete, leo hii mtu anpokuja na kusema Kikwete aendelee, hata kama mimi si mwana-CCM lakini naamini amewatukana wana CCM ambao siku ya pil yake walitakiwa waandamane kuipinga kauli ya huyu mzee! akiwatukana CCM, amekuwa kama anathubutu kwatukana watanzania wengine wote na vyama vyao vya siasa!

ana taka afe vizuri nadhani,

CCM wasipoona kauli hizi zinawatukanisha wao, sioni wala siogopi kuona kuwa karibu wana CCM wote wan mtindio wa ubongo! kazi kuwaza tumbo tu!
 


mtanzania naomba nikuulize swali.
Wakati ukijibu swali naomba ufanye kama huyu mtu hana uhusiano waki familia na mjumbe yoyote.

Tuseme dr hussein mwinyi atangaze anataka kugombea kwenye vyombo habari, fanya interview nini unadhani hii kamati inaweza kulitoa jina lake?

Nakumbuka nape nauye makelele sio mchezo, je jina la dr hussein itakuwaje?
Naomba jibu mtanzania...
 
mkuu
sasa chukulia watokee watu kama SAS,Mwandosya,Kigoda..au hata lowasa..watu wa type hiyo
halafu eti useme kikwete atapitishwa tu!!!

Mtarajiwa,

Hata mimi napenda mabadiliko lakini pia nimejifunza kuangalia jambo critically. Sasa kama hao wazee wenye majina hapo juu wanaweza wakafanya changes kwenye uongozi, itabidili niache kijiwe cha siasa.

Labda kutokea jambo kufikia hiyo 2010, ila sioni kivipi watu kama hao ambao kula yao yote inategeme rais aliyepo madarakani wamgeuke mtu huyo?

Wakitoka hapo anaanza kukamata mmoja mmoja, Chenge kwa ufisadi, Lowassa, Rostam nk.

Rais ana nguvu sana Tanzania sio rahisi kumwangusha kwa njia hiyo. Tunaweza tusipenda lakini ndio ukweli wenyewe.
 

Kweli mkuu, patakuwa hapatoshi, tuseme ukweli.Lakini wanaweza wakamvaa mzee mwinyi amshauri atoe jina!

sielewi mbona kuna majina yanayofanana na waislamu-27 na yale ya kikristo 11, hii nahisi ina nguvu sana!
 

Sijaelewa swali lako, lakini hivi unafikiri walilitoaje jina la Malecela? tena alikuwa anagombea na watu ambao sio marais. Walilitoaje jina la Bilal?

Hivi una maana huyo Dr. Mwinyi anafaa? Kwi kwi kwi!!!!
 

Kwa utaratibu huu ndio maana makundi hayawezi kwisha ccm na hopefully ita,eguka ili demokrasia ikomae zaidi.
Kama CC ndio hao hapo juu,ni wazi watamchagua JK,sasa la kushangaza kama wanajuwa kuwa wana nguvu zote hizo kelele za nini kwenye press?

Nadhani woga umeshawaingia,sasa kama hilo group jingine litaridhia grupu la mtandao liendeleze libeneke then patakuwa hapatoshi kwani siasa za visasi ni rahisi kushamiri...Haitawezekana Taifa kubadilika kama ccm itabaki kuwa ccm ile ile,mabadiliko ni lazima,historia inaonyesha hivyo....Kwamba yatakuwa ni mabadiliko mazuri ama mabaya,hilo linategemea na maamuzi ya wananchi wakati wa kupiga kura,na pia maamuzi ya wazalendo wa kweli ndani ya chama....Lakini mtanzania kwa maoni yangu,sioni ni kivipi ccm itakwepa mgogoro coming 2010,na hapo sisi ndipo tunapataka.
 

mkuu sawa kabisa tuwe critical hivyohivyo.mkuu hivi kuna ugumu gani kwa mfano kwa controversial figure kama Bilali kumgeuka Kikwete?Kula gani anayoitegemea Bilali kutoka kwa Kikwete?Huo ni mfano mmoja tu.Hata kama kuna kula wanategemea,sasa wakishammwaga Kikwete na kumuweka mtu wao kula si itaendelea kuwepo,ama?Kikwete akishaondolewa atapata wapi nguvu tena za kuwapeleka kina Chenge na Lowasa kisutu?
 

Unambwaga JK mwezi wa tano mwanzoni na kutegemea kiongozi mpya mwezi wa 11. Hiyo ya Bilali ndio sahau, si walitoa jina lake mwaka 2005, alifanya nini zaidi ya kukaa kimya?

Mimi nafikiri kitu cha kuombea ni CCM kugawanyika makundi mawili. Vinginevyo labda upinzani waweze kumshinda JK ingawaje na yenyewe kama ingelikuwa leo nafikiri uwezekano ni mdogo sana.

Tanzania tuna matatizo mengi sana kuanzia kwenye katiba. Katiba ambayo inampa rais uwezo mkubwa mno kiasi kwamba chochote anachota anaweza kufanya.

Ingeliwezekana upinzani kushinda kwenye ubunge na kuchukua nafasi ya PM ingelikuwa nzuri sana. Watanzania wangetaka kuona upande wa pili wa shilingi ukoje. Vinginevyo tutaendelea kuburuzwa tu. CCM wakiona hatari ya kushindwa inawakaribia, watabadilika. Wanatamba sasa kwasababu wana wabunge wengi mno.
 
sijaelewa swali lako, lakini hivi unafikiri walilitoaje jina la malecela? Tena alikuwa anagombea na watu ambao sio marais. Walilitoaje jina la bilal?

Hivi una maana huyo dr. Mwinyi anafaa? Kwi kwi kwi!!!!

mimi nimekupa jina la dr mwinyi wewe unaamua kumbeza, nilikua na maanisha ufukirie kama mwinyi sio baba yake wakati unajibu swali.

Jina la malecela lilitolewa na jkn na vitisho vya yeye kama atakwenda upinzani. Hamna mtu mwenye nguvu ya jkn sasa hivi, na nyakati zimebadilika.

mtanzania ngoja nikupe majina mengine maana yake la dr mwinyi ulitaki , wafuatao wakifanya press conference kujitangaza wazi, iterview na vyombo vya habari mbalimbali
salim ahmed salim, mwandosya, kigoda, mkullo, magufuli, pinda, karume.
Je hayo majina hapo juu yatazuiwa?
Kumbuka nape nauye...
 


Kwenye bold sijakuelewa mkuu.hahaha eti ya Bilali nisahau!huyu mzee ni kati ya wanasiasa ambao nawazimia sana bongo,kwahiyo siwezi kumsahau!sasa mkuu kwavile Bilali aliondolewa 2005 basi hana uwezo tena wa kumpigia kikwete kura ya HAPANA?
sawa katiba yetu mbovu,rais ana uwezo mkubwa lakini hilo unalosema la CCM kugawanyika makundi mawili ndiyo linaloweza kutokea kama mtu potential atatokea na akaachwa ashindane na Kikwete na hapo ndipo hata kama Kikwete ni mwenyekiti/rais anaweza akaondolewa vilevile.
 
- Yaaani Tanzania kweli tumefika mbali sana na hii vacuum ya uongozi wa juu, sasa tizama Shibuda naye akitafuta ushujaa katikati ya hii vacuum ya ajabu sana na yeye sio wa kwanza, tizama wengine kabla yake:-

1. Mangula - Baada ya kushindwa uenyekiti wa CCM mkowa wa Iringa, akalalama weee kua CCM imeoza na haifai ni ya mafisadi, masikini ya Mungu haya alikuja kuyaona baada ya kua katibu wa CCM for 10 years, na aliyaona pale tu aliposhindwa uchaguzi, na masikini sisi wananchi kwa kukosa mashujaa tukamshangilia kwa nguvu zote kwamba tawire!, hatukumuuliza vipi mbona hukusema kitu wakati wa Richimonduli? IPTL? RADAR? Chenge? Dowans? Kiwira? Uchaguzi wa rais 2005? Kuchafuliwa kwa Salim 2005? We arew so desparate of mashujaa kwamba it does not matter kwamba kwa nini hakusema kitu mapema kbala ya uchaguzi!

2. Msekwa - Aliposhidnwa tu uchaguzi wa Spika, akaanza kilio cha mbwa, kwamba CCM imeoza na haifai taifa linahitaji mgombea huru, again wananchi tukaamuka na kumshangilia kwa nguvu sana kwamba huyu naye ni shujaa, sasa amepewa mlo yote yale ya ushujaa yameisha, na sisi wananchi bado tunaendelea kutafuta shujaa mpya!

3. Kitine - Majuzi alitaka kununua nyumba ya serikali kule Obey, wahusika wakamkatalia, wooow! huyooo naye akakimbia kwa wananchi, haya hii CCM imeoza sana lazima zifanyike reforms, blah! blah! hao wananchi tukainuka tena vitini huyu asikilizwe huyu ni shujaa, ikatolewa order toka magogoni kuwa apewe ile nyumba haraka sana, alipoulizwa tena Kitine akasema waandishi walikosea kwa sababu hawakuripoti sawa sawa alichokisema!

4. Shibuda - Huyu naye sasa amezuka from no where, kama kawaida yetu tayari naye ni shujaa, oooh my God! What a country? What a wananchi? Shibuda alikuwa wapi siku zote kama kweli he is for real? What kama ameona ya Kitine kupewa anacholilia na yeye sasa ana yake? Kwa nini hawa waandishi hawawaulizi hawa wakuu maswali serious? Siku zote Shibuda alikuwa wapi? Amewahi kufanya nini cha maana katika uongozi wake kwa taifa? Mbona huwa hatumsikii mpaka tu wakati wa uchaguzi?

Mungu Aibariki Tanzania.

FMES.
 

of course kuna power vacuum, ndio maana tuna yaona haya, hata wakati wa Mwinyi ilitokea, na Mrema akapata Fame, mpaka Mwl aliposema tusifanye makosa au hasira tuka mpa Mrema, alizani au alifikiri Mkapa atakuwa Bado Mwanafunzi Mzuri, kumbe Chui kwenye Ngozi ya Kondo.
Kuhusu Shibuda, kama wengi walivyo sema pamoja na weakness zake, lakini ameisha onyesha hiyo nia kwenye uchaguzi uliopita i.e 2005 akashindwa na Kikwete, pia katika Kipindi cha Mkapa amekuwa anapingana na Mkapa Mara Nyingi mpaka wakaishia kumfanyia Vituko vingi ikiwemo kushushwa kwenye Treni asi hudhurie Vikao/uchaguzi wa Viongozi wa Chama. Hivyo kwa Hapa amejitahidi, lakini ameshindwa kutoka na mazingira ya CCM, sasa leo hii labda tumpine huko Jimbo kwake Kukoje? au amewafanyia Nini? Ingwaje tena kwa Tz yetu inaweza isiwe kipimo kizuri maana Nguvu zako Pekee bila ya Serikali kukusupport zinaweza kufifishwa. So at this juncture tunaweza kumu assess kutoka na tabia zake, kauli zake na wasimfu mwingine.
 

- Aliwahi kupingana na Mkapa on what mkuu? Halafu inafurahisha kusikia kutoka kwako mkuu kwamba mbunge bila serikali kuku-support zinaweza kufifishwa hilo ni jipya na ni mara ya kwanza kulisikia hapa forums kwamba kumbe bila ya support ya serikali mbunge hawezi fanya lolote la maana kwa wananchi?

- Anyways kwa kumaliza tu ni kwamba leo nimewauliza viongozi wengi ndani ya CCM, kuhusu hizi kauli za Shibuda, wakasema kwamba wamemzoea na huko ndani ya CCM hakuna kiongozi mwenye akili timamua anayeweza kulumbana na Shibuda mbele ya public, wengi wao wakasema kwamba kama haya maneno yake yangekua yametamkwa na angalau Mwandosya, wangeshituka sana, na kwamba Shibuda ana matatizo mengi sana kisiasa kwa sababu huko Shinyanga haelewani na hata makatibu kata licha ya viongozi wa juu, lakini wakakubali kwamba ni haki yake kusema maoni yake pia.

Respect.

FMES!
 
Watu lazima watumie demokrasia na uhuru wao. Suala la UTAMADUNI WA SISIEMU wa KUACHIANA ni UPUMBAVU MTUPU. Ndiyo nimesema ni upumbavu kwa sababu mambo haya ya kuachiana ndiyo yametufikisha hapa tulipo. Utumbo alioufanya Mkapa naye akamwachia JK, na yeye JK anaendelea kufanya UPUPU. Akimaliza utumbo wake naye amwachie mwingine.
Demokrasia lazima itumike iwe ndani au nje ya SISIEMU. Demokrasia isiwe kwenye makaratasi pekee, waachie watu uhuru wa kutumia demokrasia yao.
 
- Demokrasia sio kwa ajili ya uchaguzi wa rais tu, inatakiwa itumiwe na wananchi at all times, badala ya kusubiri uchaguzi wa rais tu, CCM wanaweza kufanya lolote wanalotaka as chama cha siasa, tatizo ni pale wakijaribu kutulazimisha taifa kufuata utamaduni wa chama chao CCM, then watakuwa wanakiuka demokrasia ya taifa, ninaamini kwamba so far hawajafanya hivyo.

- Unless kama inapendeza tu kurusha maneno bila political probable course.

Respect.

FMES
 
Matatizo makubwa ya nchi zetu za Kiafrika ni wale walio madarakani kutoheshimu katiba za vyama vyao au nchi zao. Huziheshimu katiba hizo kama zina maslahi kwao na mara wanapoona Katiba hazina maslahi kwao huwa wanaziruka na kuzikana ili kuzipindisha na kuendelea kulinda maslahi yao.

Tumeona umwagaji wa damu katika nchi mbali mbali za Kiafrika na hata hivi karibunijirani zetu Kenya yalitokea machafuko makubwa kwa walio madarakani kutaka kupindisha katiba ili waendelee kuwepo madarakani. Tumeona pia viongozi wakiwa kimya kabisa na mara tu wanapoona awamu zao zinakaribia ukingoni, basi hutaka katiba za nchi zao zibadilishwe haraka sana ili kulinda maslahi yao ya kuendelea kuwepo madarakani. Comandoo alitaka kulifanya hili, Museveni alilifanya na Viongozi wengi wa nchi za Kiafrika wamelifanya hili.

CCM ina taratibu zake za kumpata mgombea wa Urais toka chama hicho. Mwananchama yeyote yule ambaye anatimiza masharti yaliyowekwa na CCM anaweza kugombea nafasi hiyo. Wanachama wa CCM wana haki ya kumsikiliza mgombea mpya kuhusu sera zake na kwanini anataka kugombea wakati Rais
aliye madarakani ni wa kutoka CCM. Rais naye atawaambia wanaCCM kwamba amefanya mambo gani katika awamu yake ya kwanza ambayo yeye anayaona yanastahili kabisa kumpa awamu nyingine ya miaka mitano.
WanaCCM watayapima toka kwa wagombea hao wawili au hata kumi na kuamua ni yupi anayefaa kupewa nafasi hiyo kama mgombea toka chama chao. Wanaweza kabisa kumrudisha yule aliye madarakani au wakaamua
kuachana naye na kumteua mgombea mpya. Hizi ni taratibu ambazo ni lazima ziheshimiwe siku zote na wala zisipindishwe kwa vitisho au ubabe dhidi ya wale waliotangaza nia ya kumpinga mgombea wa CCM aliye madarakani

Tuachane na mawazo ya mgando yaliyopauka ya mwaka 47 ambayo hayaendani na wakati tulionao. Kauli za Chiligati, Msekwa Malecelea, Wazee wa Chama na wengineo wandani ya CCM kwamba wana utamaduni wao wa kumuachia Rais aliye madarakani akae vipindi viwili ni kauli potofu na zimepitwa na wakati. Tutumia vigezo vinavyoeleka ambavyo vinaweka maslahi ya Watanzania na Tanzania mbele katika kuamua ni nani anayefaa kushika usukani wa kuongoza Watanzania, na siyo hizi kauli potofu za "utamaduni wetu" ambao si ajabu ndiyo unaifanya nchi yetu isipate maendeleo ya kuridhisha miaka nenda miaka rudi pamoja na mikopo na misaada chungu nzima toka nchi wafadhili, mashirika ya kimataifa na hata bank za maendeleo duniani.

Wakati umefika Wa Watanzania kuweka pembeni unafiki na kuambiana ukweli. Kama mtu kazi imemshinda aambiwe hivyo na ushahidi uwekwe wa kushindwa kwake kazi uwekwe hadharani. Naye kama anaona amefanya mazuri basi aweke ushahidi wa mazuri aliyoyafanya hadharani halafu wanachama wa chama chake kama wanaona anastahili kurudi tena madarakani basi wana haki ya kumrudisha hata kama baadhi ya Watanzania hawataridhika na kurudu kwake, lakini taratibu walizojiwekea ndani ya chama chao kwa kupitia katiba zitakuwa zimeheshimiwa na kufuatwa bila vitisho wala ubabe. Siku zote yule asiyetaka kuheshimu katiba ya chama au ya nchi ili kulinda maslahi yake tena kwa kutumia vitisho na ubabe ni DIKTETA.

Alutta Continua!
 

sababu za kushushwa kwenye treni zilikuwa zipi? kama sio huku kuwa wamepishana na mkapa .
kuhusu kuwa sabotage mtu yoyote awe kiongozi au si kiongozi mambo yako yanaweza kubezwa au kuharibia ikiwa serikali iliopo madarakani wasinge penda kuona maendeleo yako. sasa hapa ina tegemeana na nguvu zako za kiuchumi au za kisiasa. mangeneyo itajumlisha au kutoa mwenyewe.
kuhusu kugombana na wenzie hilo lipo, lakini linategemeana na chanzo chake, je ni kupinga ufisadi au la. na hao viongozi wenzie wako kwenye payroll yanani? ni viongozi fuata upepo au independent. sasa hapa inabidi utumie akili yako binafsi kufanya analysis.
kuhusu viongozi wa juu kumuona wa maana au la hilo ni lao wamuachie basi , then ashindwe kwenye mchujo badala ya Malecela etc kuweka kiwingu au blah blah nyingi za utamaduni usio utamaduni. au tuseme utamaduni wa kudumisha ufisadi na maslahi binafsi
 
Halafu Malecela akasema ccm ni chama cha masikini,sasa hilo group hapo juu ndilo linalofanya maamuzi kwa niaba ya masikini wa ccm na Tanzania kwa ujumla....?Inashangaza sana.

Labda ulimi uliteleza alitaka kutamka kwamba CCM ni chama cha matajiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…