- Yaaani Tanzania kweli tumefika mbali sana na hii vacuum ya uongozi wa juu, sasa tizama Shibuda naye akitafuta ushujaa katikati ya hii vacuum ya ajabu sana na yeye sio wa kwanza, tizama wengine kabla yake:-
1. Mangula - Baada ya kushindwa uenyekiti wa CCM mkowa wa Iringa, akalalama weee kua CCM imeoza na haifai ni ya mafisadi, masikini ya Mungu haya alikuja kuyaona baada ya kua katibu wa CCM for 10 years, na aliyaona pale tu aliposhindwa uchaguzi, na masikini sisi wananchi kwa kukosa mashujaa tukamshangilia kwa nguvu zote kwamba tawire!, hatukumuuliza vipi mbona hukusema kitu wakati wa Richimonduli? IPTL? RADAR? Chenge? Dowans? Kiwira? Uchaguzi wa rais 2005? Kuchafuliwa kwa Salim 2005? We arew so desparate of mashujaa kwamba it does not matter kwamba kwa nini hakusema kitu mapema kbala ya uchaguzi!
2. Msekwa - Aliposhidnwa tu uchaguzi wa Spika, akaanza kilio cha mbwa, kwamba CCM imeoza na haifai taifa linahitaji mgombea huru, again wananchi tukaamuka na kumshangilia kwa nguvu sana kwamba huyu naye ni shujaa, sasa amepewa mlo yote yale ya ushujaa yameisha, na sisi wananchi bado tunaendelea kutafuta shujaa mpya!
3. Kitine - Majuzi alitaka kununua nyumba ya serikali kule Obey, wahusika wakamkatalia, wooow! huyooo naye akakimbia kwa wananchi, haya hii CCM imeoza sana lazima zifanyike reforms, blah! blah! hao wananchi tukainuka tena vitini huyu asikilizwe huyu ni shujaa, ikatolewa order toka magogoni kuwa apewe ile nyumba haraka sana, alipoulizwa tena Kitine akasema waandishi walikosea kwa sababu hawakuripoti sawa sawa alichokisema!
4. Shibuda - Huyu naye sasa amezuka from no where, kama kawaida yetu tayari naye ni shujaa, oooh my God! What a country? What a wananchi? Shibuda alikuwa wapi siku zote kama kweli he is for real? What kama ameona ya Kitine kupewa anacholilia na yeye sasa ana yake? Kwa nini hawa waandishi hawawaulizi hawa wakuu maswali serious? Siku zote Shibuda alikuwa wapi? Amewahi kufanya nini cha maana katika uongozi wake kwa taifa? Mbona huwa hatumsikii mpaka tu wakati wa uchaguzi?
Mungu Aibariki Tanzania.
FMES.