Mkandara,
Umenifanya nijibu hii hoja mapema ya utashi wangu. Sijali watakachoamua CCM, wakimchagua Kikwete sawa, wakimchagua mwingine sawa.
Ila sisi ni Taifa ambalo limeanza kujijenga katika mfumo mpya wa Demokrasia ya vyama vingi. Tumeona udhaifu uliotufikisha hapa tulipo kutumia chama kimoja na hata sasa tukiwa na vyama vingi.
Neno kuu lililotamkwa ni Utamaduni wetu, lakini je Utmaduni huu ni bora na unafaa katika Taifa linalotaka kujenga mfumo bora wa Demokrasia ambao lengo ni kuwa na uongozi na Utawala bora?
Jibu ni hapana, Utamaduni haujatusadia hata siku moja. Leo ni Kikwete, kesho ni kwenye jimbo la Ubungo, tutaambiwa tumuachie Keenja, ukija kule kwetu UK tutaambiwa tumuachie Msekwa na Mongela, kisa tuwaheshimu na ni Utamaduni.
Sasa makovu ya Utamaduni yameshakomaa hata kwenye Upinzani. Ukimpinga Mrema au Sefu, unafukuzwa uanachama, ukipingana na Mbowe, unaundiwa tume na kamati!
Sasa kama tutaendelea kusema ni Utamaduni bora, hatuoni kuwa unaleta Siasa Chafu?
Leo hii Nape aliondolewa kwa Mizengwe, mwaka 1995 waliondolewa kwa Mizengwe Kikwete, Msuya, Malecela. Mwaka 2005 waliondolewa kwa mizengwe Salim, Malecela na Dr. Bilali.
Sasa wakishaondolewa watu kwa Mizengwe, huja kauli za Utamaduni, na hivyo kumpa mtu anayeingizwa madarakani kwa Mizengwe, kibali cha kuongoza bila kupimwa kwa kipindi cha miaka 10 ndani ya chama.
Angalia Lipumba, Sefu, Mrema na Mtikila, wamekuwa wao ndio Miungu watu wa vyama vyao na huwezi thubutu kutoa neno dhidi yao kwa kuwa ni Utamaduni kuwaheshimu na kuwaachia wafanye watakalo!
Nakubaliana nawe kuwa kama kuna mwana CCM ambaye ana nia ya kweli kugombea 2010, basi achukue fomu, na aanze kampeni yake bila woga wa kutengwa na Chama.
Nao CCM kama wao ni watu wa Demokrasia, basi wajibu hoja za huyu anayegombania kuwawakilisha kwa kutaka kumuondoa Rais wa sasa na si kumtenga kwa vitisho au kutumia dola.
Leo Shibuda akija na kusema kuwa Kikwete hajafanya kazi ilivyopaswa kwa mujibu wa Ilani ya 2005, wana-CCM wamsikilize na si kumbeza kisa ni Utamaduni.
Nchi nyingi za Afrika zitashindwa kuwa na maendeleo ya kweli na Demokrasia kutokana na huu Utamaduni wa kuachiana! Anaboronga mtu, wanashindwa kumwambia kweli na kumpa upinzani kwa kuwa mtu huyo huyo ndiye anayewapa mlo na sauti.
Kama miuondo ya vyama vya Siasas Tanzania vingeachana na mfumo butu wa Wagombea kuteuliwa na CC au NEC, tungeona wigo wa fikra na kampeni ukipanuka na hivyo kuongeza Demokrasia na kujituma kwa kujizatiti.
Leo hii nikiwa alosto nikaingia Ikulu ya Dar, nina uhakika nitakaa kipindi cha miaka 10 bila wasi wasi na hata nikivurunda namna gani, hakuna atakayenotoa maana tayari kuna utamaduni.
Ni haki yao CCM kuwa na utamaduni huu, lakini je ni sawa kwa jamii yetu na wengi wetu ambao ndio wapiga kura tusio na nafasi au sauti ila kutimiza tunacholazimishwa?