Shibuda: Rais Magufuli hakufurahishwa na yaliyotendeka kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Uchaguzi Mkuu uwe wa Haki na Usawa

Hata huu ukishapita, tutasikia maneno kama haya kutoka kwa bwana shibuda.....
 
Nae ahibuda anatafuta teuzi.......tangu lini akawa msemaji wa rais. Rais ndie aliyewatuma kina jafo na genge lake la kihuni kuharibu uchaguzi na sio mara ya kwanza matukio mengi ya wazi ya kuharibu uchaguzi yamefanyika
 
Yaani hawa wasukuma wanadhani kila mtu hana akili. Alipokuwa Tabora njiani kwenda Chato hotuba aliyoitoa pale Nzega tunayo. Au Shibuda anadhani hatuna kumbukumbu?
 
Msicheze na akili za watu nyie, kwani alikuwa wapi, mbona hakuizuia hiyo sintofaham?

Naona mnataka kutuseti tu ili tupumbazike kuwa haki itachikua nafasi.

#77Neupe, #88Nyeupe, #99Nyeupe. Hadi tume huru ipatikane.
 
Huo upuuzi ameongea akiwa kabana pumzi ya tumbo ili ajistiri mbele ya watu asichafue hewa,shibuda ni mnafiki siku zote
 
Shibuda ameongea kwa niaba ya Rais?
Kama hakufurahishwa mbona hakukemea?
Ume nena vyema. Maana hata Rais alisikika akiwabeza wapinzani kwamba kususa nayo ni demokrasia.. Hayo ni maneno ya Shibuda na sio ya Jpm
 
Zimefika zama za kila mtu anajiweka karibu na waridi anukie, kila mmoja ananata na beat katika eneo lake🤣🤣🤣🤣
 
Akili
Akili zimemrudi
 
We Shibuda mambo yapo wazi kabisa....ule haukuwa uchaguzi bali uhuni...usitetee uhuni we Mzee.
 
Uchaguzi wa serikali za mitaa unasimamiwa na TAMISEMI ambayo iko chini ya Ofisi ya Rais.

Kilicho tokea sio kwamba ni kasoro hapana kusema kasoro ni kubariki uozo uliofanyika, kilicho fanyika ni kitu kilicho pangwa kwa ustadi na kuratibiwa vema nchi nzima.Wapinzani wananyimwa fomu ,watendaji wanakimbia ofisi, wapinzani fomu zao zinatupwa kwamba wameshindwa kujaza fomu, hadi unajiuliza ccm walisomea shule gani tofauti na walizo soma wapinzani?

Kama kweli angekua ameguswa na kilichotokea angechukua hatua kali kwa waliosababisha na pia angefuta uchaguzi na kufanya utaratibu mpya.

Lakini kitendo cha kujitokeza hadharani na kujivunia ushindi wa 98% wa chama chake, ni wazi yaliyo tokea yalikua na baraka zake!

Tusidanganyane ,uchaguzi ulivurugwa makusudi kabisa, na ilifanyika kwa namna inayo fanana nchi nzima.
 
Shibuda ameongea kwa niaba ya Rais?
Kama hakufurahishwa mbona hakukemea?
Haswaaa. Kama raisi alikerwa na matokeo yale ya chama chake kushinda kwa 100%, mbona hakusema hadharani wala kuiamuru tume ifanye vinginevyo?
 
"Mwanangu,laiti ungejua nguvu aliyonayo Rais"Riz1.
"Eti ashindwe kuliongelea hili!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…