shida hizi mpaka lini??

shida hizi mpaka lini??

huyo mbunge akiwaona hao wamama walivyolala hapo kweli hajickii vibaya/imani hata kidogo?...hiyo pic ya mwisho imenickitisha sana, huyo mtoto aliegeuka nyuma nae akirudi nyumbani inaonekana ametoka skul.....hapana aisee hii nchi inakera sana.
 
Ebwanaee duh hali ni mbaya inatisha duh mbunge yupo kweli sasa wangalie hao wananchi watampa huyo huyo kura.mh poleni sana duh inatia huruma kwa kweli.
 
Nyie ndy mnasikitika leo?....2 late!
Amini niliwaambia, na leo nawaambia, na hata kesho NITASEMA,
Tanzania bila KUPIGANA hatuwezi kufika popote, tunahitaji Rais kama Gen. Ghadaffi na mfumo wa wachina ndy tusonge,
La sivyo hawa mabata hawataacha kuwatafuna ndg zetu wa mashambani! HAKYAMUNGU!
 
Watanzania tuna kasumba ya kulaumu serkali tu na wabunge!! Mbunge ndio anunue hata uniform za watoto na viatu? (angalia picha ya mwisho). Bila wananchi kushirikaina na viongozi itakuwa ngumu sana kuleta mapinduzi.
Sisi kama wazazi tumefanya nini kwa watoto hawa?
 
Watanzania tuna kasumba ya kulaumu serkali tu na wabunge!! Mbunge ndio anunue hata uniform za watoto na viatu? (angalia picha ya mwisho). Bila wananchi kushirikaina na viongozi itakuwa ngumu sana kuleta mapinduzi.
Sisi kama wazazi tumefanya nini kwa watoto hawa?

Mkuu nakubalina nawe. Lakini pengine tungeweza kujifunza kutoka mifumo ya utawala ya nchi za wenzetu pia. Sera na Sheria zilizopo zinawabana wazazi kutekeleza majukumu yako. Vyombo vya Serikali vipo makini kufutilia hali bora za raia wake. Wapo wazazi ambao ni ni wazembe kulea vizuri familia lakini wapo pia wale ambao wanashindwa kutokan na sababu za kiuchumi (hao ndio asilimia kubwa). Kwa wakulima ambao mtaji wao ni nguvu zao katika kilimo, kilimo ambacho akina manufaa hata kama wakilima vipi, kamwe huwezi kukuta matatizo yanaisha iwapo Serikali haitawasaidia. Hali kashalika kwa wafanyakazi ambao wanategemea kutumika 24/7 maofsini, nguvu na akili zao zote zinatumikia Taifa hili ambalo mpaka kesho tunaimba kuwa ni "Taifa changa". Ikiwa hawa watu hawataboreshewa maslahi yanayotokana na kazi za mikono yao na Serikali yao, hakika hali itazidi kuwa ngumu milele.

Tumepoteza maeneo ya vipaumbele kupitia siasa...tukumbuke hata zile ezni za Mwl. Kulikuwa na mfumo wa kujali raia, Serikali ilikuwa ikitoa elimu na vifaa vya elimu bure, chakula kilitolewa bure kwa watotoi kuanzia chekechea, akina mama walitibiwa bure na wakati fulani hata maziwa ya watoto walipata bure. Ni kipindi kile ambapo uliweza kuona kuwepo kwa nidhamu katika ofsi za Umma, watu walijali kazi na kuthmini utu...nk. Haya yote yamepotelea wapi..Leo tunapoambiwa tuchangie elimu na huduma za jamii kama afya, maji, barabara, umeme nk, lakini bado hizo huduma zenyewe hazipatikani kabisa na kama zapatikana basi mbovu haswa.

Bado Serikali ina mchango mkubwa sana kwa watu wake kupitia Sera zake za kusaidia maendeleo.

Tujifunze toka kwa Wenzetu, mabadiliko ya kweli yatapatikana kama tutadhamiria!!!
 
Back
Top Bottom