mwanyaluke
JF-Expert Member
- Jan 22, 2015
- 704
- 2,435
Leo asubuhi nikiwa njiani nimeona ajali Moja eneo la ilula na nikiwa nimetulia napitia mitandao nimekutana na picha za ajali Ile. Ukiangalia Ile ajali Ile fuso ilikuwa imeharibika , na jamaa wa fuso walikuwa waungwana wameweka alama zote muhimu barabarani kujua huko mbele unaenda kukutana na nini, Cha ajabu dereva wa IT pamoja na alama.zote zile kalivaa Lori na matokeo yake yamekuwa magumu, ule muda tuliokuwa kwenye Lori mimi, dereva na tingo tumejadili hadi tumechoka nini kimefanya yule mwenye IT akalivamie Lori, wakati tunajadiliana na sisi tumekoswa tena na gari ndogo ya abiria amekwangua bodi, na gAri imeharibika kidogo mwenye gari inabidi atupie Milion kama Moja kwenye lile coaster ,unamuliza dereva wa coaster imekuwaje asubuhi unahama anakwambia , biashara ngumu , unamuliza kwa kukimbia hovyo hovyo ndio kunapunguza ugumu wa biashara hana majibu. Kuna shida gani kwenye akili za driver maisha magumu yanachangia au hawana tu akili ,.nashukuru Nina miaka sasa sina gari iliyojitupa kwa ujinga wa dereva, nini kifanyike kwa udereva huu wa sasa ambao unafanya barabarani kutishe , siku hizi inatisha sana unakopa, unaweka pesa kwenye gari halafu unaanza kuishi kwa hofu na kuogopa kuw huenda usimalize mkopo na gari usiwe nayo