Shida siyo maamuzi ya Kikao, wasiwasi ni kile FIFA na CAF wanawezaifanyia Ligi tu

Upekuzi101

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
478
Reaction score
1,025
Soka la bongo limepambaniwa miaka na miaka na hapa ligi yetu ilipofika kweli ni pakubwa kwakua ligi yetu ni ya tano kwa ubora Afrika na huu ni kweli kuwa kazi na uwekezaji mkubwa umefanyika. Hili lilotokea kwenye derby ya Simba na Yanga ni kosa kubwa na linaweza kutugharimu pakubwa.

Kuingiza siasa kwenye mpira ni kosa kubwa sana linaweza kusababisha hatari ya kushuka kwenye viwango vya FIFA na CAF na ikiwezekana kupigwa faini na kufungiwa miaka kadhaa. Kuna statement moja ilitolewa na kiongozi wa Bodi ya ligi kuwa mechi ilihairishwa Ili kuzuia team kushuka daraja. Japo hakuitaja ni team gani ila hayo maneno tu yanatosha kuamini kulikuwa na influence nyuma ya maamuzi hayo.

Wanasiasa wanaweza kuiharibu michezo just for their own benefit ila kaeni mkijua ligi yetu ikidharaulika, ikashushwa kwenye viwango, Karia na Bodi ya ligi mnachakitujibu sisi kama watanzania. Watu wanakaa chumbani wanapanga kuhairisha mechi kubwa namna hii bila sababu za msingi!.

Mpira ukiashaanza kuhusishwa kwenye siasa basi jua mambo lazima yaharibike maana wanasiasa siku zote wanatazama maslahi binafsi ndo maana FIFA CAF wananyima siasa kwenye michezo. Tanzania tumeshayakanyaga, maslahi ya watu wachache yanaligharimu taifa.

Bodi ya ligi na watanzania wote tukae tu mkao wa kusikilizia maana pinde tu huu mgogoro utakapoisha lazima FIFA NA CAF watatoa statement yao, sijui itakuwa nzuri kiasi gani au mbaya kiasi gani ila kiufupi siasa, bodi ya ligi na Karia, mmetuharibia mpira wetu na hamtasahaulika kwa hili.
 
Kama litaisha nchini kwa namna yoyote bila kuishirikisha CAF au FIFA, hao FIGA wanatoa wapi mandate ya kuiwajibisha TFF au Vilabu vya Simba na Yanga?
 
Mleta mada umenena vyema lkn nataka nitofautiane na wewe kidogo tu, kuahirishwa kwa mchezo No. 184 hakujasababishwa na Siasa bali ni kutokana na mahaba ya timu kwa viongozi wa umma.
Binafsi sikuona sababu yoyote ya kuahirisha game ile eti kwa sababu ya simba kuzuiwa kufanya mazoezi. Hiyo ni hoja ya kitoto kabisa ambayo mtu mwenye akili hawezi kutuelewa kwa hoja zifuatazo:-
1. Kimantiki Simba sio wageni katika uwanja wa Mkapa kiasi kwamba wagomee mech,
2. Muda waliokwenda ni kwamba walikua wamechelewa, kanuni inawataka wafanye mazoezi siku moja kabla ya mchezo wao, maana yake ni kwamba walikwenda nje ya masaa 24 kabla ya mech,
3. Katika kanuni za TFF, hawakua na 'Authority" yoyote ya kugomea mchezo ule,
4. Muda waliokua wamepewa na TFF wakufanya maandalizi ya mech hiyo No. 184 ulikua unatosha sana kwa wao kujiandaa.
Kilichofanywa na Simba kwangu naona kama vioja tu. TFF na Bodi wasipayuke kama mbayuwayu; waje na Kanuni na sio porojo za kimahaba kwenye timu zao. Hadi mama anawajua mko katika tim zipi.
Na kumbukeni mmewekera wanachama, mashabiki na wapenzi wa soka ndani na nje ya nchi.
 
Let's wait and see, kilichofanyika ni ujinga na taarifa wanazo, usidhani kwamba hawafuatilii
 
Hakika umenena vyema Ila aliyetoa statement kwa niaba ya Bodi ya ligi alisema wazi kuwa mchezo umesimamiashwa kutoka timu fulani isishuke daraja. TFF haikotoa msimamo kuhusu ligi, kuonya au kukemea mbinu zote za uvuragaji wa mechi , hii inaonyesha Bodi ya ligi na TFF lao moja, waziri nae kimya, mpaka sasa tunaona wanakimbizana na vikao. Mpira umekuwa wa vikao tena?
 
Kama litaisha nchini kwa namna yoyote bila kuishirikisha CAF au FIFA, hao FIGA wanatoa wapi mandate ya kuiwajibisha TFF au Vilabu vya Simba na Yanga?
usije ukafikiria hawafatilii wanawazoom tu!, nakukusanya data labda waamue kukaa kimya ila wakisema watumie data zao aah! kimeumana!.
 
FIFA wanafanyia kazi "Official Documents" na sio majungu ya mdomoni.
 
Wacha ifungiwe mdhamini wetu wa timu saba atanzisha ligi yake itachezewa uwanja wa Airtel!
Azam na GSM wanaweza kwenda kudhamini hata ligi za Kenya, Rwanda, DRC, Zambia au Uganda.
Watakao athirika zaidi ni vijana wetu wa ndani wanaoishi kutegemea soka.
Serikali itapoteza mapato yatokanayo na soka.
 
FIFA hawafanyi kazi kwa majungu!
Kwaiyo kilichotokea ni Majungu au ni mechi kuhairishwa bila sababu za msingi huku kukiwa na maelezo tena kutoka Bodi ya ligi kuwa ni Ili kuisaidia timu isishuke daraja
 
Back
Top Bottom