Shida ya Azam unapotazama mpira

Frustration

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3,134
Reaction score
4,124
King'amuzi pekee chenye haki ya kurusha TPL 2018/2019 ni Azam. Wanajitaidi kidogo japo walitakiwa kuongeza maboresho kaza 2a kaza, maana kamera zao hazipo powa sana ki-graphics, point of view,sharpness na clear lights.
Ila ukiachana na hayo sijaelewa hili na nadhan hapa sio teknolojia bali ni watangazaji na mafundi mitambo.
WAKATI WA MAPUMZIKO

1. KUTOENDA SAWA NA KWA WAKATI. Anaeongea(tangaza) na kuweka(switch) video ni watu wawili tofauti hasa wakati wa maonyesho ya marudio na hawasikilizani na hawaelewani. mchambuzi(mtangazaji anahitaji replay lakini anashindwa pata hadi aletewe kwa mapenzi ya wanamitambo.

2. ZOOM YA REPLAY/MARUDIO
Hapa wamefeli kabisa. Marudio yao hayana Zoom na wakizum utaona chenga. Na hata mpira wa utata au goli hauwezi kupata kitu kipya tofauti ya kile origin pindi ina stream live zaidi nawaonaga wanarudia mara nyingi zaidi (kwa matakwa sio ya muongeaji maana nae huwa anashituka na kuanza kuelezea baada ya kuona na hukatisha mada yake ghafla)

3. ACTION INAPOKARIBIA KUISHA REPLAY INAANZA .

Hapa napo sijajua tatizo nn lakini kosa hili kwao ni kawaida sana na halitatuliwi.

REPLAY ZA GOAL, MISSED GOALS AND IMPORTANT EVENTS HAWAONYESHI.
Wao wanakimbilia kuongea na team captain then hao huku wakiacha mashabiki wakiulizana hivi goli lilifungwaje?


NDANI YA UWANZA


1. OFFSIDE LINE HAMNA.
OFFSIDE haichorwi mstari kuondoa utata bali wao huwaachia macho ya watazamaji kuwa rula. Na kuzua utata usio isha baada ya mechi.

2. TEAM STARTING 11 AND SUBSTITUTES.
Panakimbizwa mchaka mchaka hapo usipime sekunde 3 wanatoa, wana mda mwingi wa kuonyesha lakini hawafanyi hivyo.

1. MPIRA WA MBALI,KONANI KAMERA HAZIZUM.
Fixed Camera zao hazina uwezo mkubwa sana kuonyesha mbali maana ukizum graphic inayokuja ni uchavu kwa hiyo wafunge jirani na maeneo hayo.


ALL IN ALL TO YOU AZAM MEDIA WHEREVER YOU ARE REMEMBER, uwekezaji hauishii hapo mlipofikia lazima muwekeze vilivyo na ukizingatia nyie ni wauzaji wakubwa wa visambusi Tanzania.
 
Unamaanisha Visimbuzi?
 
Naona Azam wanajitahidi kiasi kikubwa huwenda bado hawajapa teknolojia inayotumika kwa wenzetu.

Reply za magoli huwa zipo labda macho yako ni mabovu.
 
Kiukweli wanatia aibu sana, camera mbovu! Halafu kwenye uchambuzi hawapeani nafasi ya kuzungumza kila mmoja wao anataka azungumze, yaani ni kama klabu cha pombe walevi wanagombana.Na anayeendesha kipindi nae hataki kuwa specific kwenye kuuliza maswali kwa wachambuzi matokeo yake kila mmoja anarespond at the same moment.
Kiujumla wanafanya utumbo mwingi kiasi kwamba siwezi kuuandika hapa, sijui wamesomea chuo gani hawa watanzania wenzetu! Kama hawawezi kujirekebisha waige kwa wenzao waliowazidi kama super sports au beIn sports maana kufanya hivyo sio dhambi.
 
Ukiangalia kwa haraka, utaona kuwa wanatumia kamera chache ambazo sidhani kama zinafika nne kwa uwanja mmoja siku ya mechi.. Na ndio maana huwa kamera zinaonyesha upande mmoja tu,
ili sisi wateja wao tufaidi na tuone raha ya kuangalia ligi kuu kupitia wao AZAM basi wanapaswa wawe na kamera zinazoenyesha pande zote nne za uwanja, Nyuma ya magoli yote mawili, angle zote za kupigia kona, na picha ya juu ya uwanja...

Tusiwalaumu sana.. Pengine wingi wa majukumu ya kwenda kurekod mechi zingine mikoani linazuia, na pengine ni kutokana na uhaba wa vifaa...

Yote kwa yote, waliamua kuwekeza kuonyesha ligi ya bongo, basi wafanye kweli
 
Na matangazo yao Changia Yanga sipendi kbsa [emoji848][emoji848]
 
Taratibu tu watafika naona kila msimu wanakuja kivingine
 
Tatizo unaangalia EPL na kuilinganisha na TPL
 
Mdogomdogo watafika tu hata epl walianza kwa kuchechemea
 
Naona Azam wanajitahidi kiasi kikubwa huwenda bado hawajapa teknolojia inayotumika kwa wenzetu.

Reply za magoli huwa zipo labda macho yako ni mabovu.
Replay bila kuzumu bado haikizi mahitaji ya mtazamaji
 
Ball possession yao 56 kwa 44,nayo waibadilishe, kila mechi ni hiyo hiyo haijalishi timu zimecheza vip.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…