The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,942
- 20,077
Magufuli alipokaa miaka 6 (mwaka 2018/19 walimu waliongezewa kiasi kisichozidi elfu 10 kila mwalimu) bila nyongeza ya mishahara kwa watumishi wengine watu walimlalamikia sana.
Kwa tunaojua na kufuatilia uhalisia(facts) tulijua ni kwa nini Magufuli hakuwa anaongeza mishahara, ni kwa sababu Serikali haikuwa na uwezo wa kuongeza hata 2% ya nyongeza ya mishahara.
Hii ni kwa sababu nyongeza yoyote ya mshahara ingepandisha wage bill ya Serikali kufikia ama zaidi ya bilioni 800 kwa mwezi na Serikali ingeshindwa kujiendesha. Hili watu wa Serikali hata wizara ya fedha wanajua vizuri na hata Hagaya alikua analijua vizuri kabisa.
Simple facts ni hizi, kwanza tujue chanzo kikuu cha mapato ya serikali ni kodi, mikopo na misaada ya wahisani ama wadau wa maendeleo. Tukirudi kwenye makusanyo, TRA inakusanya wastani wa Trilioni 1.8 kwa mwezi, sawa na Trilioni 22.5 kwa mwaka.
Mishahara ya watumishi kwa mwezi ni Bilioni 700, kulipia madeni ya nje kwa mwezi ni bilioni 800 hivi, roughly jumla ni Trilioni 1.5, baki ni 300B, hapo hujatoa hela za kuendesha serikali yetu kubwa kwa mwezi ni zaidi ya hizo 300B, kwa maana nyingine hapo hakuna barabara, hakuna maji, hakuna madawa, hakuna chochote makusanyo yameisha.
Wakati huo huo una miradi ya maendeleo mikubwa kama SGR, JNHPP, na miradi mingine. Ukijumlisha vyote hivyo unaona kabisa nyongeza ya mishahara isingewezekana labda kama tungeachana na miradi ya maendeleo kama Julius Nyerere nk.
Mama yetu kwa kuyajua yote haya ukijumlisha na tozo na mikopo anayochukua sasa kama kuokota njugu lakini yeye akatumia hisia zaidi kuliko uhalisia wa kutangaza nyongeza ya mishahara ya 23% ila kwa kua facts hua hazidanganyi na hazibadiliki, ilipofika kwenye utekelezaji wakajikuta haiwezekani bora kila mtu awekewe flat rate ya 20,000 kama kifuta machozi
Miaka 6 unamuongezea mtu elfu 20 maana yake nini? Bora mngeacha tu.