Shida ya uoni hafifu

Joined
Feb 13, 2020
Posts
9
Reaction score
7
Habari ndugu zangu wanajamii, Mimi nina shida ya kuona vizuri tangu mwaka 2018, Nimeenda hospitali kama muhimili na Dr Agarwal nilipewa dawa ya vitamini wakidai ni shida ya neva za kuona. Leo hii nilkua darasani nikawa imeingia chumba chenye AC na feni macho yameanza kuniwasha sana baadae kipindi kiliisha nikatoka nilivorudi nikawa nimelala kama dk 10 nimeshituka kushika simu sioni kabisa hali imekua mbaya zaidi naomba ushauri ndugu kwa anayejua dawa ya hili tatizo au ushauri naomben jamani napata taabu sana na haya mapambano, Natanguliza shukurani.🙏
 
Hapana wakipima miwani hakuna lens inayonisaidia kuona vizuri kwani wanasema lens ya jicho haina shida, tatizo ni neva zinazo hukua taarifa kwenda kwenye ubongo
Polee sana ngoja wanakuja watakoeweza kukupa msaada ukapona ndug
 
Expert ebu nenda pale ccbrt msasani kwa wataalamu wa mambo hayo,kuwahi mapema ni jambo bora zaidi
 
Tatizo kubwa sana kwa hapa bongo madaktari walio wengi ni kama hawapo serious na kazi yao.

Nimeteseka na tatizo la sikio moja la upande wa kulia kwa muda mrefu, kila nikienda hospital wananipa dawa ya matone ya kudondoshea ,nimejitahidi kuweka dawa bila mafanikio. Sikio linapiga kelele sio za kawaida, linakuwa zito kupita maelezo, napata hisia kama limevimba lakini kiuhalisia hakuna uvimbe wowote. Sikio linasababisha kizunguzingu cha kufa mtu kiasi huwezi kuinuka ukasimama pasi na kushikilia chochote au kuwe na mtu wa kukushikilia vinginevyo unapiga kichwa chini kwa kuanguka.

Nilikutana na jamaa mmoja Bugando Hospital Mwanza ,katika kupiga nae stories nikamuelezea tatizo linalonisibu akanielekeza niende hospital ya Alamano ipo Makiungu Singida , nikaenda kukutana na madaktari walionifanyia vipimo na uchunguzi wa kina ikagundulika nasumbuliwa na ugonjwa unaojulikana kwa jina Menieres disease.

Pamoja na kuambiwa kuwa ugonjwa huu haujapatiwa tiba yake mpaka sasa lakini waliniandikia doze ya vidonge ambayo baada ya kutumia walau nilipata ahueni nikaweza kujimudu Mimi mwenyewe bila msaada wa mtu mwingine, vinginevyo ilikuwa ni patashika.

Kuna wataalamu wa matatizo yanayohusu macho pia pale Alamano. Inatakiwa uende kwa appointment na daktari vinginevyo idadi ya wagonjwa pale ni kubwa sana unaweza usionane na daktari kwa siku kadhaa
 

Pole sana.

Ni vyema ukarudi hospital kwa ajili ya uchunguzi zaidi na matibabu.

Kila la kheri.
 
Pole sana, tafuta mafuta ya nyonyo yale original uwe unapaka wakati unaenda kulala usiku juu ya macho, mpaka uone mafanikio.
 
Bawasili,kaswende,kisukari,pangusa na u.t.i ni chanzo cha tatizo kama havijapata tiba stahiki kwa muda mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…