Shida ya waamuzi haikupaswa kujadiliwa leo!

Shida ya waamuzi haikupaswa kujadiliwa leo!

Joined
Jun 10, 2017
Posts
8
Reaction score
14
Ni wakubwa kiumri, wachanga kiuongozi. TFF ilianzisha mwaka 1945 na kujiunga Uanachama wa FIFA mwaka 1964. Chama cha Soka Afrika Kusini (SAFA) kilianzishwa mwaka 1991.

Mipango mingi inayopangwa na TFF kwasasa ilipaswa kupangwa miaka mingi nyuma. Changamoto nyingi zinazojitokeza kwenye mpira wa Tanzania hivi sasa, Afrika Kusini walianza kuzishughulikia miaka ya 90s.

SAFA ilianza safari ya mafanikio na maendeleo kwa waamuzi na viongozi. Waliwatengeneza waamuzi wenye weledi na viongozi bora, lengo likiwa ni kutafuta maendeleo kuanzia kwa vijana (grassroots) mpaka kufikia ngazi ya Kitaifa.

SAFA walitafuta udhamini kwenye nyanja zote walizoamini kuwa msingi mkuu mafanikio na maendeleo ya soka. Shule za Soka, mashindano mbalimbali, ung'amuzi wa vipaji vipya, makocha sanjari na kutengeneza msingi imara wa kiuchumi. Msingi huu ulikuwa na ubunifu kupitia nyanja ya uchumi.

Uwanjani walianza na vijana chini ya umri wa miaka 12 kimashindano kwenye klabu mbalimbali ambazo zilicheza hadi hatua ya fainali kitaifa. Hawa pia waliunda timu ya timu ya taifa ya umri huo kwa udhamini wa Cadbury, mashindano hayo yalifanyika kwa mafanikio makubwa.

Kampuni ya Simba nayo ilidhamini vituo 11 vya kukuzia vijana nchi nzima na kuajiri makocha 28 ambao walikuwa na jukumu la kuzalisha vijana 60 kutoka kwenye kila kituo wataokwenda kwenye Kituo cha Soka cha SAFA.

Timu ya taifa chini ya miaka 20 ilikua ikipata fedha kutoka United Bank. Timu hii ilionesha mafanikio tangu mwaka 1997 nchini Malaysia na Morocco iliposhiriki michuano ya Dunia na Afrika.

Mwaka 1994 walianzisha timu ya taifa chini ya miaka 23 wakiwa chini ya udhamini wa kampuni ya Sasol Oil. Ilipofika mwaka 1997 kundi la wachezaji 42 walichaguliwa kutoka kwenye timu hiyo.

Hao walitakiwa kushiriki miacho ya All-Africa Games iliyopangwa kufanyika mwaka 1999 huku Afrika Kusini ikifuzu moja kwa moja kama waandaaji wa michuano hiyo iliyofanyika Johannesburg. Pia walitakiwa kushiriki Sadney Olympic mwaka 2000.

Mfumo wa kiuongozi bado ni changamoto, ni ngumu kutatua changamoto za nje kabla ya kushughulika na zile za ndani. Swala hawezi kuchomoka mdomoni mwa simba mwenye njaa.
 

Attachments

  • 20250906_141608.jpg
    20250906_141608.jpg
    178.6 KB · Views: 38
Back
Top Bottom