Shida ya Yanga ni no 9 na 10 siyo beki

ebaeban

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
2,205
Reaction score
2,697


Huyu ni beki wa AS VITA eti kasajiliwa na Yanga.

Shida kuu kwa timu ya yanga sasa hivi ni safu ya ushambuliaji ndiyo ipo butu, anatakiwa kusajiliwa straiker mwenye uwezo wa kupiga miguu yote na vichwa na pia mwenye uwezo wa kupiga faulo (freekick) na kufunga,Sarpong hana kabisa uwezo huo na anazidiwa kiufundi na wachezaji wengi wa ndani. Yanga wasianze usanii wao kuleta wachezaji wabovu wasio na uwezo na kuanza kuwapamba kwenye magazeti halafu uwanjani wanakuwa hawana jipya kama huyo Abdul razak sijui nani malizieni. sajilini no 9 na 10 wa kiwango cha afrika mashariki, safu ya ushambuliaji ndiyo hamana kitu ndo maana Yanga haina magoli mengi uwezo wao ni kufunga goli moja tu.
 
Harriet Makambo anaweza kurejea, kwa Sarpong Yanga walipigwa.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Unasema kweli mtani ila pia Kwa mpira wa Yanga ambao ndio falsafa Yao ni magoli kutokea pembeni, kama sio Kwa winger basi beki za pembeni, Kwa uchezaji wa huyo jamaa aisee atawafaa Sana, Yuko vizuri mno kwenye kutengeneza nafasi lakini pia kufunga

Laiti kama Simba isingekuwa na kapombe basi jamaa lazima hizi timu za kariakoo zingemgombania, ila Kwa uwezo wa kapombe japokuwa anazidiwa Kwa kiasi chake na jamaa sio vizuri kumletea kikosini wagombee namba hayakawii kumkuta ya Gadiel Michael Kwa Zimbwe
 
Mkuu ni kweli ila hawa Yanga bado wanahitaji beki wa kulia na kushoto mwenye viwango vya maana huwezi cheza soka la ushindani huku ukimtegemea Adeyum saleh na Kibwana shomari hao hawana uwezo wa kushindana kwa level Kama ya yanga pale.

Pia wapate beki wa kati wa maana angalau mmoja sababu tusidanganyane Yule mwamnyeto na Lamine ni wakawaida sana wale wanahitaji kupata mtu Kama Onyango pale kwenye ukuta kisha awe anacheza na mmoja wao ama Mwamnyeto/ Job au Ninja. ( Tena ikiwezekana wapatikane wawili kabisaa bado itafaa zaidi)

Wapate kiungo mkabaji mmoja wakusaidiana na mukoko pale kati wapate mtu aina ya Mkude, Fraga au Lwanga wanahitaji sana mtu wa aina hiyo kwenda kucheza na Mukoko eneo la kati. Kiukweli huwezi kaa eti unamtegemea Zawadi mauya na fei toto hao ni wakawaida mno kwa timu Kama Yanga.

Wapate pia winga mmoja was kushoto mwenye kasi ili wasaidiane na Tuisila kulia na kushoto sababu Faridi Mussa amefeli na Yacuba naye ni wakawaida sana kwenye hilo eneo.

Mwisho wapate wafungaji wawili wa maana yaani mfano wa makambo na Kagere huku wakijitahidi kumbakisha Ntibazonkiza awe backup yao.

Hapo ndo tunaweza kuiona tena yanga ile ya ushindani.
 
Sasa hapa si watasajili kikosi kizima kasoro golimshipa!!??
 
Umeongea ukweli ila kwa ntibazonkiza mmm yule gari la mkaa wiki gereji wiki road ndio maana hakuwa na timu warundi wanamjua umri wake sahihi miaka 37
 
We unawaza kisimbasimba tu think outside the box
 
We unawaza kisimbasimba tu think outside the box
Hebu waza ki yanga Yanga tuone mkuu, shida yenu ni pale mnapofikiri kila mtu ni adui yenu wakati ukweli mnaujua timu hiyo inahitaji mabadiliko makubwa
 
Umeongea ukweli ila kwa ntibazonkiza mmm yule gari la mkaa wiki gereji wiki road ndio maana hakuwa na timu warundi wanamjua umri wake sahihi miaka 37
Ni kweli kabisa mkuu umri wake ni mkubwa lakini ndio mtu hatari zaidi kwasasa pale Yanga akiwa na mpira mguuni na hata kwa mipira iliyo kufa yule bado anahitajika sana pale
 
Saidooo hafai tena
 
Misumari sio
 
Nimeoma clip zake zake chache You Tube yupo kawaida si wa kutisha sana na mpira wake upo ki-Yanga Yanga. Pasi ndefu nyingi na si mbunifu kama Show me (Kapombe). Ila ana nguvu na anakaba sana kuliko Kapombe.
I pick Kapombe over Juma.
 
Kabisa
 
Misumari sio
Hapana sina maana misumari, ispokuwa kuna changamoto Sana ya nafasi unapokuwa na wachezaji wa uwezo unaokaribiana kwenye nafasi moja, kama ilivokuwa Kwa Gadiel na Zimbwe au kipindi cha zimbwe na Asante kwasi, Zimbwe alipoteana kabisa na nafasi yake kwenda Kwa kwasi, Hadi alipokuja kocha mwingine ndio akaanza kumtumia zimbwe

kocha akiona mmoja ndio amefit kwenye mfumo wake ni ngumu Sana kubadili labda majeruhi yatokee, sasa kununua juma na ilhali Una kapombe kwahiyo lazima mmoja atakuja kuozea benchi na mbaya Zaidi anaweza kuwa kapombe maana hawa wageni waga wanakuja kikazi zaidi na wanajua majukumu yao

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…