Kwa walokole Watumishi wa Mungu kuingia ktk siasa siyo dhambi kwani tunatarajia kuona wanapeleka mafuta ya Roho Mtakatifu huko. Nchi ikitawaliwa na wenye haki (Wacha Mungu ktk Roho na kweli) Amani na Haki hutawala.
Hata hivyo, nina mashaka; kwa siasa za Tanzania? Inatakiwa uwe umesimama kiroho kweli kweli!
Kuna chombo kimoja cha habari-tafiti kiliwahi fanya uchambuzi juu ya kiwango cha uadilifu, ucha Mungu, n.k. wa waheshimiwa MPs wetu, kilisema:
70% ni washirikina; 20% ni wachawi kabisa; 5% wacha Mungu wa kweli; na 5% hawamo ktk kundi lolote la hapo juu.
Sasa, kwa jumla, Mtumishi wa Mungu unapoamua kuingia ktk arena ya siasa Tanzania, jua kabisa umemfuata SHETANI kwa uchokozi kabisa na unagusa mboni ya jicho lake! Na matokeo yake yanajulikana. Wengi wameharibikiwa kwa mahusiano ya na Bwana Yesu kuharibika kabisa!; kwa maana shetani-ibilisi hanaga masihara na binadamu kwani anajua wakati wa kutumikia adhabu yake jehanamu u karibu mno mno.
Anyway, tuendelee kuwaombea kwa bidii Watumishi wa Mungu hawa waliojitoa mhanga kwenda ku-demonstrate na kupeleka Ufalme wa Bwana Yesu Kristo bungeni.