Shigongo amuonya Diamond, amlaumu kutoza pesa nyingi shows za ndani...

Shigongo amuonya Diamond, amlaumu kutoza pesa nyingi shows za ndani...

Naona sasa kahamia kwa Kiba, ila aache kulalamika kama iPhone imekushindwa nunua techno, mwisho wa siku mkikaa wote mnaonekana mna smartphone. Shigongo na magazeti yake ni moja ya watu ambayo yanawapaga sana stress wasanii wakifulia, yanchangia sana wasanii wetu kukata tamaa, muangalie ray c, Chid Benz, Saida karoli, Mr nice nk na siku zote wao ni watu wa kuponda hasa mtu anapofall na si kumnyanyua mtu anapofall.

Mimi nina huhakika jamaa ameongeza chumvi siku zote bei ya msanii anapofanya shoo ndani inakuwa ndogo ukilinganisha na nje, tatizo jamaa anaonekana anapenda kuteleza. Naona leo kaamkia kwa kiba anamwaga sifa kibao, haya ila kiba awe makini.
 
Shigongo lazima ukubali muziki wetu umekuwa. Nakumbuka Dai alipoanza kutoza mil 10 show zake ata wasanii wenzake walisema ndio anafika mwisho lakini ona alipo sasa.
Tatizo jamaa analeta siasa kwenye issue za kiuchumi, itafika mahala bei itashuka kutokana na soko ila kwa sasa acha apige ela tu ndio wakati wake
 
huyu shigongo alizoea kitonga kutoka kwa wasanii
na kuwanyonya sasa wasanii wameanza kuamka anaanza kuisoma namba..
yeye mbona semina zake za ujasilia mali anatoza pesa nyingi tu wakati ndio zinawahusu watu wa tabaka la chini ili wajikwamue kiuchumi....

tena diamond na wasanii wengine endeleeni kukaza hadi watapike nyongo hawa wanyonyaji..
tena msikubali kupangiwa na mtu sababu wakati mnatunga hizo nyimbo hakuna aliyewashawishi,
wala hakuna aliyewasindikiza studio kurekodi
Mkuu tusiegemee upande mmoja wa shutuma tu. Mimi simtetei huyo Shigongo. Lakini kama ni kweli Diamond anatoza shs milioni 100 kwa show za Dar Live hivi ni nani kweli mtu wa chini ataingia? Ukumbi wenyewe huko uswahilini na hao kweli washabiki wa Diamond mwenyewe wa kipato cha chini watamudu kuingia pale kwa kiingilio kitakachowekwa kufidia hizo mil 100?
 
Walizoea vya kunyonga amuache diamond kama alivyo kwanza kama anampenda kwann asimwite ofisin kumshaur kama mdogo wake cc inatuhusu nn tushazoea hata insta tutamuona kwanza tangu aanze kusemwa ndo kwanza chibu anazid kuwa juu. ..halaf chibu mwenyew mafia hakubali kutumika bure na ndo inamuongezea uthaman...
 
Mjinga gani hapa Bongo alipie show ya diamond kiingilio cha 100000?
Usiwasemehe watu sema wewe hutoweza lipa....Diamond alishafanya show pale mlimani watu walilipa laki na si Diamond tuu hata Jide alishafanya pale mlimani city watu walilipa laki sasa una shangaa nini?
 
Hata miaka 2 haijaisha mmeshasahau viingilio vya Zari All White Party ?
watanzania hukumbuka ya udaku tuu lakini ya maana hawakumbuki.... hata juzi tuu jide pale mlimanicity alilipisha v.i.p laki....
 
Shigongo Diamond sio size yako tena kama uko serious tafuta wasanii size yako kina Baraka,Ben Pol,Dully Sykes,Barnaba,Chege,Harmorapa,Mwasiti,Linex uwaandalie matamasha

Last year Diamond alifanya show Iringa na Dar viingilio vilikuwa 10,000-20,000
 
...Shigongo bwege sana!
..kwa kupenda public sympathy kwa maslahi yake binafsi,hajambo!
..kama hana hela,
.akafie mbele!
 
huna hoja ya msingi. nadhani ungesoma ushauri wa shigingo kwanza ndipo utoe maoni. haya maoni yako hayana tofauti na watoa maoni ya wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu wa 2015. tatizo wabongo mihemko mingi kuliko kutafiti.
wapi ambapo hoja yangu imepwaya? Mbona yeye shigongo vitabu vyake anauza 15,000? Hiyo ndio bei mashabiki wa diamond wa mbagala live wanaiweza? Diamond kashazidi level za shigongo, shigongo aandae show za hamorapa
 
show za harmorapa Hahaha
wapi ambapo hoja yangu imepwaya? Mbona yeye shigongo vitabu vyake anauza 15,000? Hiyo ndio bei mashabiki wa diamond wa mbagala live wanaiweza? Diamond kashazidi level za shigongo, shigongo aandae show za hamorapa
 
Pesa na muda aliotumia Diamond Platinumz kutengeneza brand yake ndivyo vinavyomfanya awe anatoza kiasi kikubwa cha pesa ,maana anajua kupitia yeye income ya promoter itakuwa kubwa .He is deservin' big cash
 
Back
Top Bottom