Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Yani bado wabunge wanatuchukulia poa kiasi hiki?
===
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo, amewaeleza wananchi wa kata ya Illigamba kuwa tayari ameagiza vifaa vyake binafsi kwa ajili ya kutengeneza barabara katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.
Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo, Mhe. Shigongo amesema kuwa vifaa hivyo ni pamoja na greda, kijiko (Excavator), na malori mawili ya kubeba kokoto. Alieleza kuwa hatua hiyo inalenga kuboresha miundombinu ya barabara kwa lengo la kurahisisha usafiri na kuharakisha shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa Buchosa.
"Nimewaambia wananchi wangu kuwa nimeshaagiza vifaa vyangu binafsi kwa ajili ya kutengeneza barabara katika Jimbo la Buchosa.
Nikihutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya lligamba, nimesema vifaa hivyo ni pamoja na greda, Excavator (kijiko) na malori mawili ya kubeba kokoto". Amesema Shigongo