Elections 2010 Shigongo, Kimbisa kugombea ubunge...

Elections 2010 Shigongo, Kimbisa kugombea ubunge...

Maxence Melo

JF Founder
JF Staff
Joined
Feb 10, 2006
Posts
4,324
Reaction score
13,967
Kuna tetesi kuwa Shigongo (wa Global Publishers) na Meya Kimbisa wamechukua form kutafuta nafasi za ubunge.

Shigongo inasemekana anakwenda jimbo la Buchosa na Meya Kimbisa anaenda Jimbo la Dodoma. Kama kuna wadau wamepata uhakika wa habari hizi basi itapendeza wakatupa kwa mapana zaidi.

=========
UPDATES:

Si tetesi tena, confirmed...
 
Pale buchosa si ndio yupo yule mbunge aliyefoji vyeti anafahamika kama chitalilo, ila pia kuna enjinia dr. Mmoja naye aligombea last time anaitwa tizeba akashinda kura za maoni naye anagombea tena
 
So what happened kwa aliyefoji vyeti? TCU wapo kweli au ndio kivile? hii nchi bwana kweli tumerogwa na aliyeturoga kafa na hakuacha mrithi. Our only hope is Jesus only.
 
He
kweli siasa ni chaka la kuficha maovu na waovu.

Baada ya kuiharibu jamii kwa magazeti yake yasiyo na moral sasa shigongo ameamua kujificha nyuma ya UBUNGE!!!? najua kwa kuwa CCM inapenda watu maarufu basi watampitisha na kushiriki kuiba kura ili ashinde.
 
Shigongo naye anataka kuwa mbunge, twafwa.

Kuandika soft porn kwa teenagers na watu wenye akili zao si sawa na kuandika sheria za nchi jamani.

Ukishangaa ya Musa utaona ya firauni, mimi nilikuwa nashangaa ya Kubenea earlier this week (who is a thousand times more palatable than Shigongo, albeit with his obvious flaws) sasa nakosa nguvu kabisa nikisikia Shigongo naye eti ni contender.
 
Kamanda

Inasikitisha, lakini huwezi amini... huyu jamaa anaweza akapitishwa kugombea
 
habari khs meya kimbisa ni kweli zinarindima hapa idodomya,; tena zinadai kwamba huyo mheshimiwa ni kati ya maaspiranti 28 waliotangaza nia akiwepo mheshimiwa wa sasa, yule aliyeng'atuka 2005, na naibu meya malole aliyejiuzulu (na meya wake) miaka ya 1990 kwa sintofahamu kuhusu matumizi mabaya ya mamlaka.
 
Nami ngoja nijiandae kutangaza nia 2015:eek2:

Ishakuwa 2015 tena?
Si ulitangaza nia kwa ajili ya mwaka huu.

Anyway.
Nakumbuka Shigongo aliutaka ubunge tangu 2005.
Alimwagwa na Marehemu Amina Chifupa kwenye viti maalumu CCM.
 
Mimi nilishasema very soon itaanza Bongo mbunge search where we send the name of our favorite mbunge candidate to 1555.

Its becoming a joke mpaka ubunge wenyewe unakosa uzito. It's becomng more of a business opportunity contest " WHO WANTS TO BE A MILLI, SORRY MBUNGE?"
 
Nimesikia na Khadija Kopa yumo naye...viti maalumu!
 
Ni kweli Shigongo tagombea Ubunge jimbo la Buchosha na ameshaanza kamani za chini chini huko

Hongera sana, kila la kheri. Natumai umempiku Chitalilo kwa kuitikia "jana" na "leo" kwa miaka mingi kidogo
 
He
kweli siasa ni chaka la kuficha maovu na waovu.

Baada ya kuiharibu jamii kwa magazeti yake yasiyo na moral sasa shigongo ameamua kujificha nyuma ya UBUNGE!!!? najua kwa kuwa CCM inapenda watu maarufu basi watampitisha na kushiriki kuiba kura ili ashinde.

Du hii ni habari mbaya sana. Mtu ambaye amethibitisha wazi kuwa anatafuta hela kwa njia zote, hata ya kuharibu jamii, hata chama kitakachompa tikiti ya kugombea, inawezekana nacho kitakuwa kichafu.
 
Kweli siasa tamu.Toka uandishi mpaka siasa..Haya.karibuni sana ila huku kugumu,mwenzenu natamani kutoka ila bado nipo nipo kwanza.
 
Back
Top Bottom