Shigongo kupeleka Mahakamani sakata la "unyonyaji" wa Internet katika Bando la Mitandao ya Simu

Shigongo kupeleka Mahakamani sakata la "unyonyaji" wa Internet katika Bando la Mitandao ya Simu

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Baada ya Mfanyabiashara Maarufu 'Niffer' kuchapisha video mtandaoni kuhusu sakata la unyonyaji wa vifurushi vya internet bundle akilalamika kununua takribani GB 50 na kuisha ndani ya muda mfupi, Mbunge wa Jimbo la Buchosa Eric Shigongo amelivalia njuga sakata hilo akirejea kuwasilisha suala hilo bungeni lakini bado limekuwa tatizo kwa wananchi, hivyo anaipeleka Mahakamani ili kulipatia ufafanuzi na haki kwa wananchi wanaotumia huduma hizo za internet bundle kutoka kwa makampuni mbalimbali za simu

Soma pia
Shigongo ameandika:
"Baada ya kuongea suala hili Bungeni, bado hali inazidi kuwa mbaya! Malalamiko yanaongezeka…

Nimeamua kwa niaba ya watumiaji kulipeleka suala hili mahakamani kama walivyofanya Afrika kusini walioishitaki ICASA ambayo kwa hapa kwetu ni (TCRA) na Kampuni za simu na mahakamani, ili mahakama itusaidie kupata suluhisho ya tatizo hili, ama iagize uchunguzi maalumu ufanyike tujue kama kuna wizi ama hakuna.

Pili ielekeze kampuni za simu kwamba bando zinazonunuliwa zisife kabla ya wakati na uwepo uwezekano wa kuvuka nazo pale muda unapokwisha kama halijamalizika…

Nitakapohitaji msaada wenu watumiaji nitawapeni taarifa"
 
Ina maana serikali haijui kuwa bando zinaisha haraka? Labda wanafanya makusudi ili kupunguza idadi ya watu wasiwepo mtandaoni kupeana habari na kuhamasishana kufanya mambo ambayo ni kitisho kwa serikali
 
Hoja hiyo haifiki kokote, wenye hisa kwenye hizo kampuni ndio hao hao viongozi na wengine watengeneza viongozi.
 
Back
Top Bottom