Shigongo: Tunatoa Bilioni 200 za mikopo, tunashindwa kutoa Chanjo ya Homa ya Ini kwa Watu milioni 18?

Shigongo: Tunatoa Bilioni 200 za mikopo, tunashindwa kutoa Chanjo ya Homa ya Ini kwa Watu milioni 18?

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876


Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo, ameishauri serikali kubadilisha mwelekeo wa kibajeti katika Sekta ya Afya kwa kuwekeza fedha nyingi zaidi kwenye tiba za kinga (preventative medicine) kuliko tiba za kuponya magonjwa. Ameyasema hayo leo, Mei 12, 2026, alipokuwa akichangia makadirio ya bajeti ya Wizara ya Afya.

Shigongo alianza mchango wake kwa kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa vituo vya afya na zahanati katika jimbo lake, huku akiendelea kuiomba serikali kuwapatia gari la wagonjwa la majini (boat ambulance) ili kuhudumia wananchi wa visiwani. Pia, amempongeza Waziri wa Afya, Mhe. Mchengerwa, Naibu Waziri, na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kwa utendaji wao kazi mzuri.

Maendeleo ya Sekta ya Afya Tangu Uhuru, Shigongo alibainisha mafanikio makubwa ambayo taifa limeyapata katika sekta ya afya kwa kulinganisha takwimu za Mwaka 1961 na sasa:
  • Idadi ya vituo vya afya imeongezeka kutoka vituo 22 pekee mwaka 1961 hadi kufikia 1,361 hivi sasa.
  • Zahanati zimeongezeka kutoka 700 mwaka 1961 hadi 8,714.
  • Idadi ya madaktari wa Kitanzania imepanda kutoka madaktari 13 mwaka 1961 hadi kufikia 12,000.
  • Umri wa kuishi wa Mtanzania umeongezeka kutoka miaka 37 mwaka 1961 hadi miaka 67, kiwango ambacho ni cha juu ukilinganisha na nchi jirani ambazo umri wao wa kuishi ni miaka 66 na 65.
Wito wa Kuongeza Bajeti ya Kinga, Licha ya mafanikio hayo ya kimuundombinu, Shigongo aliikosoa bajeti iliyowasilishwa kwa kutotenga fedha za kutosha kwenye kinga.
  • Amekumbusha kuwa misingi iliyowekwa na Rais wa Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere, na Waziri wa Afya wa kwanza, Derek Bryceson, baada ya kupata uhuru ilitilia mkazo mambo matatu: kuwekeza kwenye kinga, kufundisha wataalam, na kupanua miundombinu.
  • Amemuomba Waziri Mchengerwa kurekebisha bajeti hiyo ili kuelekeza fedha nyingi zaidi kwenye kinga kwa sababu "bila kinga taifa haliweszi kuwa taifa bora."
  • Vilevile, aliishauri serikali kuongeza bajeti ya afya ili kufikia asilimia 15 inayopendekezwa na Azimio la Abuja, akibainisha kuwa kwa sasa Tanzania inatenga takriban asilimia 7 pekee.
Mapambano Dhidi ya Homa ya Ini (Hepatitis B), Akizungumzia mapambano ya Homa ya Ini ambayo amekuwa akiyafanya tangu mwaka 2014, Shigongo alitoa mchanganuo wa jinsi serikali inavyoweza kulinda Watanzania dhidi ya ugonjwa huo:
  • Ili kulinda taifa, asilimia 90 ya watu (ambao ni takriban milioni 58 kati ya Watanzania milioni 65) wanapaswa kupata kinga.
  • Kutokana na uamuzi wa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa wa mwaka 2002 kuanzisha chanjo kwa watoto, takriban asilimia 70 ya kundi lengwa (vijana wa chini ya miaka 25) tayari wana kinga.
  • Amesema mzigo uliobaki kwa serikali ni kuwachanja Watanzania milioni 18 pekee ambao hawana kinga.
  • Ameshauri serikali kutafuta ruzuku kutoka taasisi kama GAVI au Center for Disease Analysis Foundation (CDAF) ambazo zinaweza kushusha bei ya chanjo hiyo kwa ununuzi wa jumla hadi TZS 1,350 kwa dozi, hivyo kufanya dozi zote tatu kugharimu TZS 4,030 pekee kwa mtu mmoja.
Msimamo Mkabidhi wa 'Chanjo ya Kuzaliwa' (Birth Dose), Shigongo alihitimisha mchango wake kwa kutoa msimamo mkali kuhusu chanjo ya Homa ya Ini kwa watoto wachanga mara wanapozaliwa (Birth Dose).
  • Ameeleza kuwa chanjo ya 'Pentavalent' inayotolewa sasa hufanyika mtoto akiwa na wiki sita, jambo linalomuweka mtoto kwenye hatari ya kuambukizwa na mama mwenye ugonjwa huo tangu siku ya kwanza anapozaliwa hadi kufikia hizo wiki sita.
  • Akibainisha kuwa nchi nyingine za Afrika kama Misri na Ethiopia tayari zinatoa chanjo hiyo mara tu mtoto anapozaliwa, Shigongo alimtaka Waziri kuja na majibu ya kuridhisha kuhusu utengaji wa bajeti ya chanjo hiyo (Birth Dose).
  • Akitamatisha, aliweka wazi nia yake ya "kukamata shilingi" endapo Waziri hatoeleza ni kiasi gani kimetengwa kwa ajili ya chanjo hiyo kwa watoto wachanga.
 
Ila ingekuwa habari ya umbea sasa!!
Hakuna habari ya umbeya ndefu hivyo ndio maana zinasomwa we unadhani mtu kutwa nzima ana fanya kazi kachoka anaweza kusoma gazeti lefu hivyo labda weekend
 
Back
Top Bottom