Shiilingi ya Tanzania yachungulia kaburi

MPadmire

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
3,957
Reaction score
3,245
Oooohoooo, watanzania kwishney

Thamani ya shilingi yazidi kuporomoka dhidi ya US $.

Bei za vitu zitazidi kupanda bei

Kipato cha mtanzania kipo pale pale au kipato kinaweza kupungua.

Sasa Tanzania tumefika pabaya, haya ni matokeo ya kutowajibika na ufisadi

Mission town (kimjini mjini)

Watoto wa vigogo wachache wananeemeka wakati mamillioni ya watanzania wanataabika
 
imefikia kiasi gani sasahivi...??dah tena usiniambie nisje nkalia!!
 
kina william @new york city ??
 

Tunakoelekea sio kuzuri...soon tatakuwa hatuna tofauti na kwa mzee Mugabe.
 
leo arusha usd 1 - tzs 1520 mpaka tzs 1525 hakika inatisha


Mkuu naona umequote ndogo. CRDB sasa wanauza hadi sh 1550 pamoja na bank nyingine. Hawa serikali wasichukulie mzaha jambo hili, kwani siku watu wakisema basi sijui tutakmbilia wapi.
 
HIZI NI RATE ZA NBC YAANI NI NOMA TUPU NANGOJA J3 SIO ITAFIKA WAPI
As of 21 May 2011

Spot
Buying​
Seling​
USD
1,475.92​
1,560.92​
EUR
2,098.71​
2,255.67​
GBP
2,393.68​
2,559.76​
AUD
1,546.22​
1,662.23​
 
Leo nimepita bureau de change,sikuamini macho yangu!1Usd ni Tshs 1,547!nilikua nataka vidola vyangu ikabd niwe mpole tuu.
 
Sasa hao washauri wa rais wa uchumi mnaowasifia na wengine sijui wamepata tuzo za world economic forum (wef) wanafanya nini???????????
 
Tunakoelekea sio kuzuri...soon tatakuwa hatuna tofauti na kwa mzee Mugabe.

Mkuu pamoja na purukushani na vituko vya Mzee Mugabe, kitakwimu za IMF inaonekana Zimbabbwe iko juu kwa Tanzania. Wenzetu wana mtu makini kwenye wizara muhimu na sekta nyeti kama Wizara ya Fedha, Benki Kuu na Wizara ya Mipango. Huku kwetu Waziri wa Fedha nasikia kule NBAA amesajiliwa kama mhitimu wa NAD kwa vile alikeli ACCA kule London. Naye Profesa Ndollu yupo usingizini tu wala hajui kinachoendelea
 
Ki-msingi kuna factor nyingi zinapelekea fedha to depreciate {kushuka thamani} ikiwa ni pamoja na export Vs Import factor! Deficit budget etc! Tatizo kubwa serikali yetu haipendi kuwatumia wataalam wa Uchumi! Na badala yake wameamua kuwatumia ndugu zao ambao wameshindwa kufanya kazi ipasavyo!
 
Huko Spain, watu wako kwenye uwanja wakidai mageuzi, hali bora ya maisha na ajira!
 
Na bado, si hatutaki kujianzishia maandamano wenyewe ya kupinga huu ujinga.
 
Mkuu naona umequote ndogo. CRDB sasa wanauza hadi sh 1550 pamoja na bank nyingine. Hawa serikali wasichukulie mzaha jambo hili, kwani siku watu wakisema basi sijui tutakmbilia wapi.

Kwani serikali tunayo basi?
 
kina william @new york city ??

mkuu, unataka kumwamsha huyu mrithi mtarajiwa wa mali za kifisadi za tingatinga aje humu kuchafua hali ya hewa kuwatetea warithi wenzie wa mali chafi zenye damu za watanzania akina riz 1, jan makamba , nepi nauye, huseni ruksa et al?
 
tulitegemea nini kama hatuzalishi, hatuuzi nje na ile ndogo tuliyo nayo tunaitumia vibaya? sasa hivi petrol ni 2100 Tsh. Ila nawapongeza watanzania kuwa waelewa, wapole, na wenye kukubaliana na hali hata iwe mbaya namna gani. Hongereni watanzania wote!

Pia nawapongeza viongozi wetu wanaozidi kuagiza mashangingi kwa fedha za kigeni badala ya matrekta imara; naipongezaa serikali ya CCM kwa kuendelea kuwarundikia vyeo wale maafisa wa serikali ambao taarifa zilizowekwa wazi ni kuwa wameshiriki au wamechangia kuingiza nchi katika mikataba feki (rejea ripoti ya mwakyembe na uteuzi wa Mr. Mrindoko).
 
acheni kupoteza muda kwa kupiga kelele. Ongezeni uzalishaji. Watu hawafanyi kazi, sasa hivi vyama vya siasa vingeamua kuweka mkakati maalum wa kuhimiza Watanzania kufanya kazi. Mara maandamano, wizi maofisini, mara kuvuana magamba. Tusidanganyane hapa, uchumi hauwezi kuinuka km watu wanakula rushwa na hawazalishi.
 
Hello Anfaal,

Kama mkulima anazalisha sana ila kuna panya buku (wanavunia shambani) na panya wa kawaida (wanavunia ghalani) je huyo mkulima ataiona faida ya juhudi zake za kufanya kazi??????

Watanzania wanafanya kazi, wanatozwa kodi mbili mbili (PAYE na VAT) halafu tunaingia mikataba feki ya Umeme na kufilisi kodi za watanzania. Je huoni tatizo hapo....

Au unaona NAPE NNAUYE ana sera yoyote ya kumsaidia mtanzania yeyote? Sera ipi NNAUYE anayo? Sema hapa JF.

Tunaachia Madini kwa wakwe zetu (wawekezaji) kwa 10%....

Tunawapa wawekezaji Ardhi kubwa, watanzania wanakuwa wamachinga. NNAUYE ni kijana gani asiyejali vijana wenzake, anachumia Tumbo lake tuu. Viongozi wa CCM wanamiliki viwanja kila mkoa na mashamba makubwa makubwa.

Kumbuka kisa cha mashamba kule BURKA, RIZ 1 amerudisha yale mashamba?? Lowasa amerudisha. Kimei (o) wa CRDB

NAPE anashambulia mkombozi wa watanzania, Shujaa anayewafumbua watanzania macho. NAPE unataka watanzania waendelee kulala ili uendelee kushiba na kuvimbiwa???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…