Shikamoo Alikiba, shikamoo Diamond!

Shikamoo Alikiba, shikamoo Diamond!

Hapo mlengwa mkuu ni Diamond platnumz kwa huu Uzi na siyo Ali Kiba.
Huja balance hata kidogo umeegemea upande mmoja ndugu,Sijajua imewaza nini au X_Mass ulikula matikiti.
nadhani itakua zaid ya matikiti maana mm nilikula ugali mlenda xmas lakin nawaza fresh tu sio kama hiv.
ahahahaha
 
AliKiba:
huyu jamaa ni mwanamuziki mzuri kwakweli. anafanya kazi kivyake na hana shobo za kijingajinga. anatoa nyimbo anapoona inafaa kufanya hivyo. anapondwa kweli humu JF na watu wanaojiita ni magreat thinkers. ukiziangalia sana sababu zenyewe za kupondwa kwake, utagundua kuwa shida ni wivu, chuki, ushamba, kukosa akili, kukosa kazi za kufanya, kuchanganyikiwa na hali ngumu ya maisha kutokana na bro magu kubana sana, ushabiki wa kijinga,kufake ugreat thinker, shobo na kufuata mkumbo!! pamoja na yote hayo, jamaa (alikiba) yuko cool na anapiga kazi tu kwa kadiri anavyojaaliwa na Muumba. pesa ya kula anatengeneza, tena ya kuwazidi wengi tu humu!!

shikamooo kubwa kwako alikiba.

diamond:
huyu jamaa ni mwanamuziki hodari kabisa. anajua kukitumia kipaji chake vema tu katika kujitengenezea mpunga. hakati tamaa na amefanikiwa kuviruka viunzi kadhaa vya watu waliojaribu kumkwamisha. humu JF anapendwa mno na kila anachofanya lazima asifiwe sana tu. hata wimbo wa BABA LAO nao ulisifiwa sana na kuonekana kuwa ni wimbo bora kabisa. ana uswahili flani kama kupenda kurusharusha vijembe kwa wenzake n.k.
nampa shikamoo kwa ujanja wake uliotukuka wa kuweza kuwabadilisha watu kijanja sana. alipoona watu wengi humu wanamchukia makonda basi akatumia ufahamu wa kupendwa kwake humu kubadilisha hilo. alikuja na wimbo wa BABA LAO na humo akawaambia wanaJF kuwa makonda na mwakyembe ni mababa yao.....sasa wamelikubali hilo na wanauimba huo wimbo vizuri na kwa heshima kubwa.

alipoona watu wanamchukia sana tulia ackson humu, juzi akaenda huko mbeya kupokelewa nae.......sasa hivi wanaJF wako bize kurusha threads za kuzungumzia kukubaliwa kwa tulia na uwezekano wake mkubwa wa kumng'oa Sugu.

huko nyuma, wakati wa sakata la vyeti na habari za bashite zimepamba moto humu JF, aliwahi kutoa kibao 'bora nikae kimya' ambako moja ya mistari yake aliwashangaa watu (JF bila shaka) wakibishana tu mambo ya vyeti badala ya kwenda kutafuta senti. ghafla wanaJF wakatulia na kubaki wakiuimba huo wimbo.

shikamoo diamond!!!
Mtoe kiba hapo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka ndio umeanza huu badala ya kukaa na kuwaza ni namna gani tutatoboa kimaisha, tunakwenda kuwajadili watu wenye mafanikio yao!! Vijana tunafeli wapi?!!

ᴮʸ cₐᵣₑₑₘ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿᵈ
 
Mwaka ndio umeanza huu badala ya kukaa na kuwaza ni namna gani tutatoboa kimaisha, tunakwenda kuwajadili watu wenye mafanikio yao!! Vijana tunafeli wapi?!!

ᴮʸ cₐᵣₑₑₘ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿᵈ
ha ha ha ha ha!
vyuma kaka, kila kitu bado kiko vile vile.....jobs, spouse and targets remain the same, only the calendar has changed!
 
Back
Top Bottom