Shikamoo kilimo

ankol

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2012
Posts
2,355
Reaction score
4,260
Nilitenga milioni kumi. Ndiyo 10m!.
Nikaingia porini. Niliweka watu wakasafisha pori. Hiyo ilikua December last year.
Ila kila nikikaa machale yananicheza.
Page pendwa yangu ikawa tma.
Yes bila hiyana nikasoma kua mvua zitanyesha chini ya wastani.
Refer hapa.
Basi nikajipa moyo. Nikaendelea na process za kulima na kisha ilinyesha mvua kidogo. Tukazika mbegu shamba lote.
Ekari 30.
Tuliweka camp nikiambatana na wafanyakazi wangu wa mkataba wa 3.
Vibarua hawakukauka shambani kwangu.
Kwakweli kazi ilifanyika kwa ustadi wote.
Sikutaka kurudi mjini mpaka nione hatima ya pesa yangu ninayoizika siku hadi siku.
Huku nikipewa matumaini na wakulima wenzangu kua mvua ziko karibuni.
Siku zinakatika jua linazidi kudhoofisha mimea yangu.
Inasikitisha sana kushuhudia mimea inanifia machoni mwangu.
Nimekata tamaa.
Inasikitisha sana.
 
Pole sana.

Kuna mdau alisema eti yeye kazi anayofanya haitaki kuwa na mvua,hivyo mvua kutokunyesha anaona sawa tu. Kilimo kikianguka,upatikanaji wa vyakula ukapungua,sekta zote zitatikisika. Mtu hawezi kufanya kazi wakati tumboni ana njaa.

Kutafuta suluhisho la huu ukame unaonyemelea,ni jukumu la Kila mmoja hata kama sio mkulima.
 
Niliona nakumbuka lakini siku kufuatilia kama ulikuwa na MILION kumi ulitakiwa uchimbe kisima Chako na ununue pampu ya solar kipindi hiki Cha jua inafanya kazi vyema sana Kisha mipira ya kazaa ya kusambazA maji katika Eka 5 tu asee ungepiga mazao hiyo tulishaacha kipindi Cha nyuma huko jitahidi kishirikiana na watu
 
Kuna ule uzi ulileta mwanzo, wadau wakakuuliza umelima wapi ? Ni zao gani unapanga kulima? Ili ushauriwe humu ndani kuna wazoefu wa kila nyanja,,,, ukakaza fuvu hata hukujibu,,,, kula chuma hicho, next time toa taarifa inayoeleweka ili watu wajue pa kukushauri !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…