Shikamoo kilimo

mkuu pole sana ungefanya utaratibu wa umwagiliaji drip irrigation imekuwa mkombozi wa wengi eneo dogo lakini output ni kubwa.
Unajua unachoongea?
Ushawahi uguza mimea ikiwa impigwa na uhaba wa mvua.
Unaelewa mdau aksema 10m imeenda?
 
Reactions: 2v1
Kweli kabisa mvua imetuumiza sana lakini kwa mkulima wa kweli hii ni changamoto kama changamoto nyingine. Huwezi kumsikia anasema hatokuja kulima tena na vikauli vingine vya kimama mama kama hivyo huwezi kumsikia.

Wait for a comeback its always there, very soon. Kwaresma njema
 
Bora nikanywe ngano tu...nawasaidia wakulima kupata soko.
 
Yes. Niliwekeza 10m kwa kulima eka 30.
Ingeenda poa ningevuna na kupata wastani wa 1m kwa eka.
Hiyo si pdf, ni real figure niliishuhudia misimu miwili iliyopita.
Means total ningevuna 30m ndani ya miezi sita.
Sasa kama bado uko vizuri usikimbie huko shambani
 
Wewe nae una shida mahala,hivi unaweza fanya kilimo Cha biashara kwenye Mikoa ambayo Haina uhakika wa mvua?

Kama unataka kilimo biashara nenda Mikoa ya Ruvuma, Morogoro Kusini,Njombe, Mbeya,Songwe,Rukwa,Kigoma na Katavi.

Huko walau huwezi poteza hela Yako yote hata kama imetokea bahati mbaya ya mvua nyingi au kuwahi kukata kiti ambacho ni nadra sana ila hela Yako utarudi hata bila faida.

Mwisho nimejifunza kwamba mradi wowote ukipania na kuweka malengo makubwa Huwa unafeli,Ili ufaulu Unatakiwa kurudia ndipo uta graduate hiyo stage.Pole sana.

Kilimo ni kamari bet kiasi ambacho uko tayari kukipoteza Ili ikitokea uweze ku recover.

Bora Ufugaji una nafuu kiasi.
 
Hiyo ilikua December last year.
Mwenendo wa mvua za vuli ulitolewa September 2024 ikionyesha zitakuwa chini ya kiwango. Wewe hadi December ulikuwa hujafuatilia tu na uko kwenye industry ya kilimo?
 
Kilimo hawawekezi kias kama hicho kama ni mgeni. Just with laki tatu
 
pole sana
kilimo nakipenda sana lakini kwa zaidi ya miaka mitatu sasa sijalima baada ya kutopata mafanikio tarajiwa kwa misimu miwili mfululizo nikaona nipumzike kidogo.
japo mwakani natamani kurudi tena.
tulia! mshukuru MWENYEZI MUNGU atakupa kwa jinsi nyingine kwakuwa kwa uwekezaji wako katika kilimo wako watu uliwaokoa na kuwapa nafuu ya maisha katika kipindi unafanya kilimo naimani hakuna utakachopungukiwa utapewa kwa njia nyingine.
bora wewe umejaribu kwenye kilimo wako watu hiyo hela wametumia kwa usiku mmoja na marafiki lakni kwako umeajiri kuna watu walitumia fedha yako kuwanunulia watoto mahitaji ya shule pia chakula.
hakika tulia utaiona faida yake kwa namna nyingine na wakati mwingine utasimama na utafanikiwa zaidi
MWENYEZI MUNGU azikumbuke sadaka zako zote na akutete tena.
 
Ha! kweli? milion kumi zingetosha kwa kilimo cha umwagiliaji kwa ekari tano? pamoja na miundo mbinu yote ya kisasa!? ni wapi huko nasi tujaribu.
 
Kilimo chataka moyo!
Nadhan n muda sasa kwetu wakulima kuikumbatia teknolojia tu. Kutegemea mvua ni kujidanganya.
 
P0oe mkuu
Kama unajitafuta kwenye kilimo usilime mikoa yenye mvua haba

Lima Njombe
Mbey
Songea
Rukwa sio pote
Mkuu mda huu Njombe zinapiga ila sio pote ila zimenyesha za kutosha.
Nimepanda maharwge siku ya tano leo inanyesha nying sana.
Siwezi hama Njombe, kumebarikiwa sana mvua labda ntakapo acha kilimo.
 
Ikinyesha panda mihogo, mtama au dengu.Haya mazao yanastahimili ukam.
Usipoteze kabisa mtaji panda hayo mazao hayanaga shida na mvua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…