Shikamoo kweli zinaboa

uajekundu

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2016
Posts
541
Reaction score
461
Habari wanajamvi,
Leo nataka kuongelea hizi shikamoo ambayo ni salamu maarufu Tanzania. Nna miaka 26 nafanyakazi taasisi fulani ya Serikali, sasa ofisi yetu imeleta wanafunzi wa field/ practical training wengi sana, kinachoboa ni zile shikamoo zao hasubui ..yani mabinti na wakaka ambao bado wako chuo sawa, tunapishana miaka miwili, mitatu hadi minne yanajitia matoto yakikuona tu eti shikamoo....ukweli hii salamu inaboa haswaa unaposalimiwa na mkubwa mwenzio.

Nna apriciate hii salamu nikisalimiwa na watoto wadogo, kuanzia form 4 kwenda chini kwa levo yangu, atlist kidogo ina make sense hata mi naskia raha kuitikia shikamoo ya mtt.

Sasa unakuta binti kubwaa limeshazalishwa huko chuo limenenepeana linaanza na shikamoo zake.

Zamani nilikua siwaelewi wasiopenda hii salamu ila sasa naelewa.
Nisalimie shikamoo kama nimekupita 10 yrs less than that, hata habari, mambo, za kwako inakua mzuka..shikamoo zitoke kwa vibaby.khaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
unapewa shikamoo mkuu unyimwe hiyo riziki au unataka kuzeeshwa
 
Wengne wanasema shkamoo znawazeesha

Sent using Jamii Forums mobile app from my Android phone
 
Kesho wakikuamkia tena, wajibu Mambo? Watapata ujumbe kuwa hupendi shikamoo.
Ukiangalia sio wote wanapenda kuitoa sema ni mazoea tuliyokuzwa nayo.
 
Wamayo kinehe shi nanho??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi hii naipenda itolewe tena na watoto tu ile anasema kamoo anakushika kichwani na hata kama umesimama kako chini kanajaribu kunyosha mkono ili akushike kichwani inabidi uchuchumae kidogo.. its just soo lovely..ila sasa hawa wakubwa hata mie nakuwa uncomfortable.. ananipa shkamoo naipotezea namwambia mambo vipi
 
asee ili lipo sana yaani unakuta mtu hata ni mkubwa kuliko wewe lakini kwasababu yuko field eti shkamoo dada,,wanakera hatarii sijui wanashindwa nini kusema hata goodmorning
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…