Shikamoo master tactics "Gamond"

mwehu ndama

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
630
Reaction score
2,151
Binafsi sare ya 0-0 dhidi ya timu ya wachambuzi (Ubuntu botho) sio matokeo niliyokuwa nikiyataka sababu niliamini Yanga sc, tulikuwa na nafasi ya kushinda huu mchezo kibabe, tena katika style ya soka la kisiasa, söka la malengo na sio kukimbia kimbia tu kama kondoo aliyekatwa kichwa "kibu Denis"

katika mazingira ya mchezo wetu wa jana ambao tuliwakosa wachezaji wetu muhimu 3, ni wazi timu ilihitaji kubadilika kimbinu ili kuweza kupambana na Masandawana pamoja na jeshi lao la wachambuzi kina jemedari saidi, wilson oruma na geof lea bila kusahau sapoti kubwa walokuwa wakiipata toka kwa mashabiki hoehae nchini toka mbumbumbu efusii.

Ni katika suala la mbinu ndipo Gamond alipomuonyesha bwana mdogo Rhulan mokwena kwamba kuna madaraja ya ubora katika Kila taaluma, na ni yeye Grand wizard "Gamond" ndie alieshika usukani wa mechi hapo jana.

Akiwa na kikosi chake ambacho wanajangwani wengi tulikitilia shaka hasa kutokana na kutokuwepo kwa baadhi ya nyota wetu, bado gamond aliwachezesha mamelod katika biti yake aliyotaka, kuna muda aliwaacha wapige vipasi ushuzi vyao katika eneo lao, then anawakamata kati, afu kuna muda tulikuwa tunafungua turbo, wakitaka kufungua mechi tu, tunawapoza tena, yaan kwa kifupi mamelod jana walikuwa frustrated dakika zote 90 "hawakujua cha kufanya wakabaki wanasubiri bahati nasibu wakati huo huo Yanga inawapiga counter attacks za kibabe, inshort Rhulan Mokwena alikuwa katika mifuko ya Gamond jana.

Sikuwah kuhisi Gamond ambae ni muumini wa falsafa ya kushambulia anaweza kubadilika na kuja na mbinu kali na hatari kama ya jana,. Kwa kifupi huyu ni kocha wa viwango vya dunia na chini ya usimamizi wake, sina mashaka na mechi ya mkondo wa pili pale Pretoria, na nafikiri baada ya hii mechi, CAF na wafuasi wao watakoma na kuacha kabisa kufix droo zao na kuzipambanisha timu zao pendwa na timu za Tanzania kwa kuhisi watapata mteremko

Viva Yanga Africa, kudos Gamond, daima mbele nyuma mwiko
 
Hamna Kitu Pale, South Africa
Watapigwa Tuu
 
Kuna mtoto humu anaitwa - Dany - anampinga sana Gamond, .....ana viposti vyake humu akimkanyagia Gamond, ....kama analijua soccer vizuri basi game ya jana Gamondi kamthibitishia kuwa yeye ni kocha wa viwango gani.
 
Wilson oruma amekubali mziki wa Jana wa yanga .
Yanga walitengeneza hatari za kufunga (clear chances )kati ya 7 na 10 hii peke yake Imebeba maana kubwa .
Mamelodi hii ilibeba kombe la afl na kufika nusu fainali ya caf na kujaza wachezaji 9 starting line up Kwenye bafana Bafana ya Afcon .
 

Pacome kutokucheza ndio kipona Kwa yanga! Angekuwepo pacome yanga wangeshawishika kufunguka na hapo ndipo wangekutana na dhoruba ya magoli!! Pacome si chochote mbele ya mamelodi!! Subirini kmc!!
Viva Yanga Africa, kudos Gamond, daima mbele nyuma mwiko
 
Kiukweli kwa ile mechi maua yote apewe Gamondi. Mimi baada ya kikosi kile kutoka niliinama chini kwa hofu, sikuamini mpaka tunaenda mapumziko 0-0 na hakukuwa na hatari yoyote kuja upande wetu.

Gamondi ametoa somo jinsi ya kucheza mechi za mtoano, tuombe kheri mechi ijayo nyota wetu warejee tufuzu nusu fainali.
 
Ulichokiona ndicho ulichokiongea mkuu. Umeongea kila kitu. Wengi hatukudhani kwa kikosi kile,hasa baada ya kuwakosa nyota watatu,kwamba tutawakamata vile wale masandawana.

Gamond ni bonge la kocha. Tuwashukuru pia wachezaji wetu kwa kufuata kwa ukamilifu maelekezo ya kocha. Pale mbele wangeongeza umakini kidogo tu,yale maamuzi ya haraka kwenye eneo hatari,tungewapata vizuri wale.
Tuombe tu mechi ya ijumaa wawe wamepona kwa 💯 nyota japo wawili tu,Pacome na Aucho
 
Hiii imeenda

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…