mwehu ndama
JF-Expert Member
- Nov 12, 2019
- 630
- 2,151
Binafsi sare ya 0-0 dhidi ya timu ya wachambuzi (Ubuntu botho) sio matokeo niliyokuwa nikiyataka sababu niliamini Yanga sc, tulikuwa na nafasi ya kushinda huu mchezo kibabe, tena katika style ya soka la kisiasa, söka la malengo na sio kukimbia kimbia tu kama kondoo aliyekatwa kichwa "kibu Denis"
katika mazingira ya mchezo wetu wa jana ambao tuliwakosa wachezaji wetu muhimu 3, ni wazi timu ilihitaji kubadilika kimbinu ili kuweza kupambana na Masandawana pamoja na jeshi lao la wachambuzi kina jemedari saidi, wilson oruma na geof lea bila kusahau sapoti kubwa walokuwa wakiipata toka kwa mashabiki hoehae nchini toka mbumbumbu efusii.
Ni katika suala la mbinu ndipo Gamond alipomuonyesha bwana mdogo Rhulan mokwena kwamba kuna madaraja ya ubora katika Kila taaluma, na ni yeye Grand wizard "Gamond" ndie alieshika usukani wa mechi hapo jana.
Akiwa na kikosi chake ambacho wanajangwani wengi tulikitilia shaka hasa kutokana na kutokuwepo kwa baadhi ya nyota wetu, bado gamond aliwachezesha mamelod katika biti yake aliyotaka, kuna muda aliwaacha wapige vipasi ushuzi vyao katika eneo lao, then anawakamata kati, afu kuna muda tulikuwa tunafungua turbo, wakitaka kufungua mechi tu, tunawapoza tena, yaan kwa kifupi mamelod jana walikuwa frustrated dakika zote 90 "hawakujua cha kufanya wakabaki wanasubiri bahati nasibu wakati huo huo Yanga inawapiga counter attacks za kibabe, inshort Rhulan Mokwena alikuwa katika mifuko ya Gamond jana.
Sikuwah kuhisi Gamond ambae ni muumini wa falsafa ya kushambulia anaweza kubadilika na kuja na mbinu kali na hatari kama ya jana,. Kwa kifupi huyu ni kocha wa viwango vya dunia na chini ya usimamizi wake, sina mashaka na mechi ya mkondo wa pili pale Pretoria, na nafikiri baada ya hii mechi, CAF na wafuasi wao watakoma na kuacha kabisa kufix droo zao na kuzipambanisha timu zao pendwa na timu za Tanzania kwa kuhisi watapata mteremko
Viva Yanga Africa, kudos Gamond, daima mbele nyuma mwiko