Shikamoo wasanii wa bongo, naomba mnijibu maswali yangu

Status
Not open for further replies.

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
1.Mimi nashindwa kuwaelewa kabisa, Hivi ni kweli nyie ni mambo safi? Yaani hela mnazo za kutosha au wanawazushia?
2.Hivi ni kweli zile picha za uchi ninazo ziona kwenye mitandao ya kijamii na magazeti ni kweli au wanawasingizia?
3.Hizo nyumba ninazosikia mnajenga, wengine nasikia wanasema wananyumba nne, je ni kweli ni zenu au ni za kuzugia kibongobongo ili maisha yaende? Kama ni zenu kwanini bado mnakaa nyumba za kupanga?


4.Samahani kwa maswali yangu, nia yangu ni kutaka kutoamini watu wanayo yasema.
Kuna watu nliona na kuhakikisha wanayo yafanya ni kweli Mfano, Mhogo mchungu na Kingwendu wana nyumba kule Mbagala, Ney wa Mitego ana nyumba, Masanja joti na Mpoki, vengu, wakuvwanga wana nyumba japo bado baadhi yao hawajamalizia, Madee anagari na kashanipa lifti.


Lady jay dee ana nyumba ana range ana kampuni, Juma nature ana nyumba na benz, Matonya alijengewa na Barabuu japo yeye kamalizia so ni nyumba yake ipo Tanga, Prof.Jay ana nyumba Kimara na gari Mbili. Marehemu Kanumba alikua na gari, Ray wa bongo movie ana gari na Mke(chuchu hans) wanaishi pamoja sijajua kama kaoa kihalali sababu huyu mwanamke alikua mke wa mtu.


Dully sykes aka Mr Misifa anamiliki nyumba Tabata ana gari aina Honda anamiriki studio pia(Dhahabu records). Afande Sele kajenga Morogoro.

Ndugu zangu Wasanii, Kuna baadhi yenu sijui wanachokifanya.

1.Diamond nasikia ana hela yaani utajiri unao karibia billion, Kanunua Mtaa Kijitonyama Makumbusho, ana nyumba nne. Hivi haya maneno ni kweli?
Mfano juzi kati alipiga picha kwamba Kanunua V8 kumbe gari ni ya Papa Chifu Kiumbe.

Diamond ana nyumba nne lakini Mbona Mama yake Hamhamishi Pale Tandale Kila siku ya Mafuriko maji yanaingi Ndani?. Kaka Diamond anasema anahela na wasanii wengine lakini Mbona bado amepanga? Kwanini Hajakamilisha nyumba japo moja tu ahamie?

Diamond anasema ana hela, Mbona wacheza show wake Wanaishi Maisha ya dhiki kiasi kwamba kwenda makwao wanaenda kwa kujificha. Wacheza show wapo nane, kwenye hiyo billion ameshindwa kutoa hata mil 50 japo awanunulie magari used?. Anazidiwa na Nyandu tozi anayesomesha Ndugu zake sekondari karibia watoto sita.

Kaka diamond anasema Kanunua Mtaa Makumbusho, Mbona mbona akienda kwa Wema gari anapaki nje?

2.Wema Sepetu sidhani kama kweli Mambo safi, ananitia Mashaka kwa sababu Mara ya kwanza alisema amejenga nyumba Kijitonyama kumbe nyumba ni ya Mama Ngoma Mwisho wa siku akahama na sasa yupo Makumbusho. Siku za nyuma alidanganya Kanunua Gari aina ya AUDI na akawa ananipita eti hi figganigga lakini Mwisho wa siku Akaja kunyang'anywa pale Maeneo ya Namanga na Kampuni ya Majembe sababu gari ilikua ya Kaka CK(Clement huyu anayetembea na Kajala) na alikua hajamaliza kuilipia alipoinunua. Yani ile Gari Clement akua hajamaliza deni kwa mtu aliyemuuzia. Baada ya Kunyan'ganywa Diamond akasema atamnunulia V8. Hadi leo sijaona V8.

Kama Wema na Diamond wangekua na Hela wangeshindwa kulipia kipindi chao cha IN MY SHOES cha channel 5 hadi kimefungwa na Wanadaiwa bado. Kweli wana hela?

Nimetaja hawa baadhi sababu ndio Habari ya Mjini. Naomba Mniondoe ushamba wangu jamani, Hizi hela zenu wasanii Mnaosema Mnahela, Mmeziweka wapi? Au ni kipi cha maana Ambacho mumefanya. Sioni chochote zaidi ya kununua vinywaji, nguo, kuazima Magari, Majungu na Umbea. Naomba mnifafanulie hela zilipo.

Hivi Adamu Mchomvu, Bwana yake Aisha akirudi toka majuu si utaumbuka? Kwatu wote Mjini wanajua unaendesha Magari ya demu. Mnatutia aibu bwana.

Ingependeza Mtu aishi maisha yake kama Anavyo fanya B12. B12 Angalau anajitahidi ana duka pale Mwenge japo wateja sasa wamepungua sababu ya kuhamisha kituo cha basi lakini Maisha kapiga bao. Hana nyodo anatoa hai kwa washikaji. Nia yangu ujirudi kwa sababu umri unaenda na dogo kashaanza shule.

Nyie Bongo Movie Hela zenu zipo wapi? Watu wanashindwa hata kuwasaidia sababu wanajua Mnahela kumbe weupe.
Nawapenda Sana ndugu zangu. Mia
 
Kwingine kooote umezunguka tu BT hapa mlengwa diamond.!!!yaaan ni sheeeda..tutwaslia wenzako wakija
 
hapo kwa Adamu umeleta uongo,Adam Mchomvu ana gari yake ndio anatembelea,halafu Aisha Mchomvu ni mke halali wa Adam,,jama ni mpiganaji sana tofauti na unavyomsikia radion au kwenye vijiwe
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…