Shikamoo wewe kipofu uliyeniibia pikipiki na ukaiendesha

Ila wezi wa aina hii wananifurahisha sana,hongera sana we dada uliofundishwa bodaboda hongera na we babu kipofu,mi mshabiki wenu.

Wezi wa namna hii hadi unawaonea wivu, wanatumia akili hadi unatamani bora wangekuibia wewe... utabaki ukijicheka tu.
 
Huo wizi upo sana, ila mara nyingi hua wanapanda mwanamke na mwamaume halafu mdada andosndosha kiatu halafu wanakuomba ushuke uwaokotee, hilo vumbi lake watalokuachia sio la nchi hii.
 
Mwenzako aliangushiwa gongo la kilema pikipiki ikaenda yeye akabaki na gongo.
 
Kwa bei uliyowapa ya book 3 Magomeni hadi Manzese, wewe sio dereva wa boda boda na hii hadithi umetunga maana hata bei za boda huzijui.

Na kama ni kweli wewe ni dereva wa bodaboda unawapiga watu kwa bei ya kitapeli kama hiyo na tena kipofu - ulistahili kuibiwa, karma hiyo!
 
Kuna jamaa aliibiwa piki piki yake maeneo ruaha(anakofanyia shughuli zake) ilimuuma sana akaelekezwa kwa mtaalam pale mahenge morogoro. Yule mama alimwambia usijali baba we endelea shughuli zako. Baada ya siku3 jamaa alieiba aliipeleka mwenyewe kituo cha polisi pale ruaha na akasema anamtafuta sana mwenye nayo... kwa iyo njia za kupata mali zako zipo... kuwa na connection tu.
 
Huwezi ukaanza bei ya chini kwenye biashara za kuelewana bei,nilimwmbia 3000 lakini hata angesema ana buku jero ningeenda (Ulemavu sio sababu ya kulipa nauli ndogo kwangu)
 
Aisee dah mkuu nipo ifakara sahizi lakini nilishaamua kumuachia Mungu
 
Huwezi ukaanza bei ya chini kwenye biashara za kuelewana bei,nilimwmbia 3000 lakini hata angesema ana buku jero ningeenda (Ulemavu sio sababu ya kulipa nauli ndogo kwangu)
Huwezi kuanza na 3000 kwenye nauli ya 1000. HUo ni utapeli tu. Vipi kama ni mgeni, si utamwibngiza mjini. Kwanza kwa nini usimwambie nauli inayotozwa, kwa nini utarajie mbishane kwanza ndio mkubaliane?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…