Shikamoo zimekuwa nyingi mpaka nahisi utu uzima mbona mapema sana

Shikamoo zimekuwa nyingi mpaka nahisi utu uzima mbona mapema sana

Ungekuwa na gari usingezipata hizo shikamo.

Katafute hela nunua ata Premio wacha ujinga kijana
 
Ndugu zangu wana Jamiii hizi shikamoo kutoka kwa vijana wa dogo wa form 4 au wa vets zimekuwa nyingi mpaka nachanganyikiwa .inafika kipindi naitika kwa kuibia ibia mana nahisi kama bado sio mkubwa kivile wa kupewa shikamoo za kila mara.kwahiyo sasa wakuu tunafanye kuepuka hizi shikamoo?

Au tukubali tu kuwa mwendo tushaumaliza?

Au tuanze kuvaa vipensi kujifanya tupo kwenye makuzi?

Au tunyoe viduku ili mtaa utuone watu wa hivyo na tukose heshima?

Ila ngazi tatu sio poa watanzania.

I hate shikamoo
Shikamoo ni salamu ya kishamba na ni ishara ya utumwa
 
Au tukubali tu kuwa mwendo tushaumaliza?

I hate shikamoo
Wakati ukuta; ukipigana nao utaumia mwenyewe.
Kubali umri wako wala usiukatae, maana hata ukiukataa hautarudi nyuma.
Wanaadamu tunapenda kuishi miaka mingi, lakini eti hatupendi kuzeeka!! Hii itawezekanaje?
Usipopenda kuzeeka, basi usiishi miaka mingi; ukiweza, aga dunia ukiwa na miaka kati ya 30 na 35 kwa wanawake; na kwa wanaume kati ya 40 na 45.
Uzee hutuijia kisogoni, hatuwezi kuuona; utastukia watu wa wewe kuwapa shikamoo wanazidi kupungua siku kwa siku, wale wanaokupa wewe shikamoo wanazidi kuongezeka siku kwa siku; hapo ujue kumekuchwa, jua linaelekea kuzama😱🙆
Jina lake ni WAKATI ⏰⌚; anasogeza sekunde, dakika, saa, siku, wiki, mwezi, mwaka, 🗓️ 📆 muongo, Karne, milenia. Hajawahi kusimama tangu dunia imeumbwa.
Unapofurahia MWAKA MPYA tambua kwamba huenda ukawa ndio mwaka wako wa kuondoka duniani; hapa tuko matembezi, hatuna mji udumuo.⚰️
 
Back
Top Bottom