Shikamoo zimekuwa nyingi mpaka nahisi utu uzima mbona mapema sana

Ungekuwa na gari usingezipata hizo shikamo.

Katafute hela nunua ata Premio wacha ujinga kijana
 
Shikamoo ni salamu ya kishamba na ni ishara ya utumwa
 
Au tukubali tu kuwa mwendo tushaumaliza?

I hate shikamoo
Wakati ukuta; ukipigana nao utaumia mwenyewe.
Kubali umri wako wala usiukatae, maana hata ukiukataa hautarudi nyuma.
Wanaadamu tunapenda kuishi miaka mingi, lakini eti hatupendi kuzeeka!! Hii itawezekanaje?
Usipopenda kuzeeka, basi usiishi miaka mingi; ukiweza, aga dunia ukiwa na miaka kati ya 30 na 35 kwa wanawake; na kwa wanaume kati ya 40 na 45.
Uzee hutuijia kisogoni, hatuwezi kuuona; utastukia watu wa wewe kuwapa shikamoo wanazidi kupungua siku kwa siku, wale wanaokupa wewe shikamoo wanazidi kuongezeka siku kwa siku; hapo ujue kumekuchwa, jua linaelekea kuzama😱🙆
Jina lake ni WAKATI ⏰⌚; anasogeza sekunde, dakika, saa, siku, wiki, mwezi, mwaka, 🗓️ 📆 muongo, Karne, milenia. Hajawahi kusimama tangu dunia imeumbwa.
Unapofurahia MWAKA MPYA tambua kwamba huenda ukawa ndio mwaka wako wa kuondoka duniani; hapa tuko matembezi, hatuna mji udumuo.⚰️
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…