Shilatu amefanya ziara kujiridhisha uhalisia wa upatikanaji wa chakula kwa Wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari zilizopo Tarafa ya Mihambwe

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
510
Reaction score
839
Na Mwandishi wetu Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amefanya ziara kujiridhisha uhalisia wa upatikanaji wa chakula kwa Wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari zilizopo Tarafa ya Mihambwe ambapo ameridhishwa na upatikanaji huo wa chakula lishe kwa Wanafunzi.

Gavana Shilatu alijionea uhalisia Wanafunzi wakipewa kifungua kinywa, chakula cha mchana na chakula cha usiku kwa wa walio hostel ambapo alitoa pongezi kwa hatua hiyo kubwa ya uzingatiaji lishe kwa Wanafunzi.

"Napenda niwapongeze Wazazi na Waalimu kwa namna wanavyoendelea na utaratibu wa kuzingatia suala la lishe kwa Wanafunzi. Upatikanaji chakula unaimarisha elimu na afya kwa Mtoto. Ni jukumu la kila mdau wa elimu kuhakikisha lishe inazingatiwa kwa Wanafunzi kutokana na umuhimu wake." Alisema Gavana Shilatu mara baada ya ziara.

Serikali nchini ilitoa mwongozo kupitia Wizara ya Elimu kuhakikisha Wanafunzi wote wanapatiwa lishe shuleni kwa ajili kuimarisha elimu na afya Jambo ambalo linatekelezwa vyema kwa shule zote za msingi na sekondari zilizopo Tarafa ya Mihambwe.

 
Shilatu alitarajia ukuu wa wilaya kabla Mungu hajafanya yake, pole sana ngosha ngosha
 
Na hii nayo ni habari?
 
Gavana waTaifa ndugu yetu Shilatu, kambi popote kaka endelea kupambana. Hao wanaokuponda kisa Ugavana potezea kaka.
 
Anajitahidi kutembelea
Hivi ofisini huwa anakaa kufanya kazi saa ngapi
 
Hua wanafanya hivyo kiongozi wakiwa wanakuja...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…