Shilingi 500 bandia zimezagaa mtaani tuwe makini

ivanmark714

Member
Joined
Jul 13, 2019
Posts
67
Reaction score
110
Habari,

Wana JF mimi sina utaalamu wa uwandishi hivyo tuvumiliane kwa wale wakosoaji wa uwandishi.

Twende kwenye lengo, hivi karibuni kumezuka mia 500 fake nyingi sana mtaani, ambapo mwisho leo usiku huu nimekutana nayo na nikathibisha madai haya niliyowahi kusikia kabla.

Utaijuaje ni fake? Ni nyepesi mno, inang'aa sana, ni kubwa kwa umbo ukilinganisha na pesa halali, zile tarakimu 500 hazibadiliki kwa ndani kuja neno B.O.T.

Hivyo Serikali kupitia B.O.T na mamlaka zake nyengine waliangalie hili, na wananchi tuzidishe umakini katika hili.

NB: Naomba radhi kwa uwandishi mbovu lakini ujumbe umefika.
 
Ndo zile yule jamaa wa Zanzibar anaonekana ana macho makubwa.?
 
Hivi,huwa mnajuaje kama ninyi si waandishi wazuri?Yaani mtu aliyelogwa anamjua hadi mchawi wake!
 
Uwandishi.... bila picha?
 
Hili nalo mkaliangalie..
 
wengi watapuuza kama walivyopuuza maono ya ajali ya ndege ya abiria.

Mamlaka husika zilifanyie kazi suala hili.
 
Hakuna usimamizi soko limerudi kuwa huria
 
 
Habari,

Wana JF mimi sina utaalamu wa uwandishi hivyo tuvumiliane kwa wale wakosoaji wa uwandishi...
Acha watu wapate maisha. Mbona hauongelei jinsi tulivyosaini mktaba wa 69bilioni wa kununua software ya kufuatilia kukatika tu kwa umeme na bado ungeendelea kukatika Sana.

Acha wanaume wapo kazini wanatumia akili watokeje Kama vile vile wamejichukulia shares zao za gesi na kwenye madini mpaka jpm alilia jinsi Nchi inavyoliwa na watu wachache mno.

Gesi alitaka azalishie umeme mwingi ili tuwe na viwanda ikashindikana akakimbilia bwawa la nyerere mana gesi Sheria inataka tuinunue Tena na ilhali Ni ya kwetu.

Yaani Kuna kasee hii nchi kameiuza kinyama,kameua watu mno sema huwezi ona,unajua Ni wangapi wanafariki na mimba kisa hakuna huduma nzuri za hospital eneo alilopo anashindwa kujifungua vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…