Shilingi hiyooooo yaporomoka

Hili likitokea kutakuwa na vilio vya kusaga meno kwani bidhaa muhimu hazitashikika kwa bei kubwa.
Kwa sera hizi, mikurupuko hii, u much know wa sasa, lazima tufike huko. Labda itasaidia kuamsha watu wengi.
 
Reactions: BAK
Tatizo Mzee baba alidhani kuongoza inchi ni kutesa wapinzani
 
Hivi huyu jiwe ni unskilled and illiterate Mbona kila anachofanya hafanikiwi .
Our dear leader is a PhD educated and he knows what he is doing.
Uchumi wa nchi yetu unaendelea kuimarika siku hadi siku, na maisha ya watanzania wanyonge yanazidi kuimarika na kuwa bora zaidi. I am very proud of stigglers gorge, reli ya standard geji na mabasi ya mwendokasi, na super highway ya njia 12 mpaka chalinze.
Tembeeni vifua mbele because we are on the right track to becoming a donor country.
Wapiga dili awamu hii imekula kwenu 😛
 
One the most important statement I noted there, why did they savagely crack them down?
I really don’t know! All I know is the negative impact or the consequences of the decision.
 
Reactions: Qwy
Mhn! Kaazi kweli kweli!
 
Shortsighted regime, don't they have people in their circle who are at least capable of anticipating the aftermath of those types of imbecile moves?
I really don’t know! All I know is the negative impact or the consequences of the decision.
 
Shortsighted regime, don't they have people in their circle who are at least capable of anticipating the reparations of those types of imbecile moves?
A good and a valid question!
 
Reactions: Qwy
tusubiri kidogo low season ya utalii yaja (April&may) wote tutanena
 
Nataka Magufuli ashindwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Jamani tusitupe jongoo na mti wake". Wala tusilete siasa kwenye masuala ambayo hayahitaji siasa ila busara na hekima.
Mtakumbuka kuwa Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani Tanzania ilipata sifa kubwa ki-mataifa na tukasifiwa kweli kweli. Tatizo likitokea kwenye nchi zao, watu wakawa wanajiuliza, "Magufuli angefanya nini kupata suluhu ya jambo hilo?" Watu wengi hasa wasomi wetu, wanapenda sana kuelezea matatizo kutumia vitabu vinasema nini. Acheni vitabu rudini kwenye historia ya nchi yetu mtagundua kinachotokea.
Tanzania tuliwahi kuwa na mfumo ambao Serikali ilikuwa inahodhi maamuzi ya kiuchumi. Nia yake ilikuwa njema lakini mfumo huo una mapungufu kwa sababu wale wanaomua masuala ya uchumi hawawezi kuwa na taarifa za kutosha na kwa muda mfupi kiasi cha kutimiza matakwa ya nchi nzima. Hapo unakuwa umeamini kuwa watu wanaofanya maamuzi hayo wote wana nia moja na nia njema ya kufaidisha umma ambayo si kweli, kuna unafiki, uwongo na upendeleo mwingi ambao huingiliana na nia njema iliyokusudiwa. Ndiyo hulka ya binadamu ilivyo. Mfumo wa aina hiyo hatimaye hauwezi kutumia rasilimali zake kwa ufanisi kwa hiyo mwishowe huwa mzigo hata kwa wananchi. Mfumo huu tuliujaribu wakati wa Chama kimoja ukatushinda.
Mfumo uliokuja badala yake ulikuwa na nia ya kutawanya madaraka ya uamuzi ambao sisi tuliita "kulegeza masharti ya kiuchumi." Huu mfumo ndiyo ukaturudisha kwenye uchumi wa sasa na Tanzania tukawa sehemu ya uchumi wa dunia. Ilikuwa kazi kweli kukubalika, kama inavyotokea Zimbabwe sasa na Venezuela itakuwa hivyo hivyo mwishowe, ingawa wenzetu wana mafuta mengi.
Katika kulegeza masharti, Tanzania ilianza kujijengea mfumo wa kiuchumi ambao ulifanana na nchi nyingine na mfumo huo ulilenga kuwa na taratibu za kisheria na taasisi huru kwa mujibu wa sheria ambazo zinatumika kwenye nchi mbali mbali. Huu mfumo ulipoanza kukolea hapa nchini ndipo uwekezaji wa ndani na nje ukaanza kukua kwa kasi.
Mfumo huu unahitaji utawala thabiti hasa kuanzia juu kabisa kwa Rais. Mtakumbuka wakati huo ndipo hata Mahakama Kuu ilianzisha Idara ya Mahakama inayohusika na masuala ya Uchumi na Biashara, Kituo cha Uwekezaji kilianzishwa na hata Mamlaka za Udhibiti zilianzishwa. Nia ilikuwa kuwahakikishia wananchi na Ulimwengu kuwa utawala wa sheria hata kwenye uchumi utakuwepo.
Katika nchi yo yote, Tanzania ikiwemo, mapigo ya moyo wa nchi hutegemea sana mapigo ya moyo wa kiongozi mkuu na katika nchi yetu ni mapigo ya moyo wa Rais wetu.
Kwa hiyo katika awamu zote, hasa tangu awamu zote mpaka sasa tumetegemea mapigo ya Rais aliyepo madarakani.
Kuna wakati ambapo, pamoja na sheria na taasisi kuwepo, rushwa na ufisadi ulianza kuingilia ufanisi wa taasisi. Baadhi ya maamuzi ya mahakama, kwa mfano yalipendelea watu wenye fedha, kama huna fedha hukuweza kushinda kesi. Baadhi ya watu wenye uhusiano na watawala walianza nao kuwa na kauli kama vile ni watawala na ukibishana nao kweli ulikuwa unapatwa na balaa kama vile umebishana na mtawala mwenyewe! Hili liliwaudhi wananchi wengi hata wageni ambao walikuwa wanaitakia Tanzania mema. Kwa hiyo awamu ya tano ilipokuja ikakemea rushwa na ufisadi kwa nguvu, watu wote wa ndani na nje walifurahi. Na hata kwenye taasisi za kiuchumi sasa hakuna mtu ambaye si mtawala anatamba siku hizi.
Hali ya sasa ilivyotokea ni kwamba, kwa nia njema kabisa, ili kuzuia ufisadi, maamuzi makubwa ya uchumi yamerudi karibu kama awamu ya kwanza. Matatizo ni yale yale kuwa taarifa na maamuzi hayawezi kuwa ya haraka kama uchumi unavyotaka. Pia Taasisi zimeingia uwoga wa kufanya maamuzi. Kwa mfano, kodi zimekusanywa mahali pengine ambapo siyo halali. Wawekezaji wa ndani na nje hawana uhakika kama utawala wa sheria unasimamiwa kwa uhuru. Hakuna kitu ambacho mwekezaji anachukia kama kuamka kesho na kusikia Waziri amebadili utekelezaji wa jambo fulani bila ama majadiliano au kutoa notisi inayotakiwa. Masuala uwekezaji si ya "kufuata sheria bila shuruti" ni suala la utashi wa mtu binafsi kama atumie hela kwenye anasa au awekeze kwa faida ya miaka ijayo. Lazima mwekezaji huyo afikirie ajali zinazoweza kutokea kwa wakati ujao.
Kwa hiyo Tanzania kama inataka iendeleze pale wenzake walipokuwa wamefikia, ukiondoa rushwa na ufisadi, inatakiwa irudishe imani kwa wananchi na wawekezaji kuwa:
1.Utawala wa sheria utakuwepo na utaonekana hata kwa mjinga kuwa upo.
2.Taasisi zenye uhuru wa kiundeshaji ziachiwe uhuru huo na zionekane zina uhuru pamoja na kufuatwa taratibu za uteuzi kwa mujibu wa sheria na uteuzi usiwe zawadi ya jambo lo lote maana uteuzi wa aina hiyo unampa kiburi aliyeteuliwa. Aidha,hizi taasisi zina namna ya kuwawajibisha wanaofanya makosa makubwa kama ilivyo kwa Rais mwenyewe; lazima taratibu hizo zifuatwe wanapowajibishwa vinginevyo wataendesha mambo kwa kutazama uso wa Rais na kujaribu kumpendeza badala ya kutenda haki.
3.Weledi, uelewa, uzoefu na uaminifu ndiyo viwe vigezo vya uteuzi na siyo shahada peke yake.
4. Kodi ni lazima ikusanywe; lakini iwe kwa mujibu wa sheria. Kuna makampuni ya kimataifa ambayo ni ya wezi hayo yachujwe; lakini kuna makampuni hapa duniani yanaendeshwa kwa mujibu wa sheria na yanasisitiza kulipa kodi kwenye nchi ambayo yamefanya faida. Kama hawajaiba tuwape heshima yao. Ndiyo maana wenzetu wengine kwenye nchi zilizoendelea hata wosia wa urithi hawaachii watoto wao sehemu kubwa ili nao watoto wafanye kazi kama wazazi wao walivyofanya. Wanatoa sehemu ya urithi wao kwenye nchi zetu. Wastaarabu wenye mali halali huwaita wanaokwepa kulipa kodi halali "moonlighters" yaani wafanyia kazi kwa mbalamwezi. Tusidhani kila mtu wa nje ni mwizi! Ukiamini hivyo basi usichukie unapoambiwa na Wazungu kichaa kuwa kila mtu mweusi ni mwongo!
Mwisho, ombi kwa serikali ni kushikilia bango la ufisadi kama inavyofanya sasa, lakini kutumia utawala wa sheria, haki, bila ubaguzi, bila visasi vya aina yo yote na kutambua kuwa ili nchi iendelee huhitaji wanasiasa tu unahitaji kada nyingi zifanye kazi kwa uzalendo na imani kuwa hapa ni mahali salama ambapo hisia za mtu siyo zinazotawala ila sheria. Watu hawatatoa hela nje watazibakiza humu ndani. Ikiwa watu wa kawaida hawanunui dola na kutoa nje basi mauzo ya nje yanayolega lega yatakuwa mambo ya muda tu kama Benki Kuu inavyoeleza. Lakini tukirudi kule kwenye miaka ya 1960 na 70 uchumi wetu hautakuja kutengemaa. Watu, hasa wenye kipato cha kati wakibaki na mchecheto kila fursa ya kununua dola na kuwekeza nje, nyingine hata kwa marafiki tu zitatafutwa na shilingi itaendelea kudorora kama ilvyofanya zamani kutoka Dola moja shillingi 8 mpaka sasa ni shillingi 2,240!
 
...shilingi itaendelea kudorora kama ilivyofanya zamani kutoka Dola moja shillingi 8 mpaka sasa ni shillingi 2,240!
Wakati Jumuiya ua Afrika Mashariki inavunjika mwaka 1977, dola moja ya Marekani ilikuwa sawa na shilingi 7/= ya Tanzania, pound sterling ya Uingereza ilikuwa sawa na shilingi 20/= ya Tanzania (na ndio maana noti yetu ya 20/= iliitwa pauni moja), shilingi moja ya Kenya ilikuwa sawa na shilingi moja ya Tanzania.

Hivi leo dola moja ya Marekani inakaribia sh. 2,500/= , pound sterling ya Uingereza imevuka sh. 3,000/= na shilingi moja ya Kenya inakaribia sh. 25/=. Mwaka 1977 ndio CCM ya sasa ilizaliwa na haihitaji akili kujua kuwa CCM ndio adui namba wani wa taifa hili.
 
We need some miracles,in deed mr stone up to now still conservative.Tutakufa kichaga na cash mfukoni.we have alot of resources but the problem how to run.but this round amebaki na penalty moja akikosa lazima tuwapigie wachina magoti watupe hela zao za moto ata kama riba ipo juu.mambo yamekuwa mengiii,na mengi......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…