Shilingi mia tano imekuwa kero mtaani, maduka ya jumla wengi hawataki kuzipokea

Shilingi mia tano imekuwa kero mtaani, maduka ya jumla wengi hawataki kuzipokea

Mapensho star

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2016
Posts
3,052
Reaction score
4,104
Tangia mabadiliko yafanyike ya pesa ya shilingi mia tano mwanzo ilikuwa ni noti lakini sasa ni sarafu, changamoto tunayoipata wananchi ni kwamba hii pesa imekuwa ni kero hasa zikiwa nyingi wenye maduka ya jumla wengi hawataki kupokea.

Hivyo kusababisha kutokuingiza kwenye mzunguko; Mfano mimi hapa ninazo elfu 50 lakini nashindwa kufanya manunuzi ya msingi kutokana na changamoto hiyo.
 
Kukataa kupokea pesa halali ni kosa la kisheria na lina adhabu yake.
 
Hata mimi sipendi hela za sarafu sijui kwanini! Yaani nikizipata huwa naomba nibadilishane na mtu anipe noti au nitanunua chochote ili tu nisikae nazo!
 
Hata mimi sipendi hela za sarafu sijui kwanini! Yaani nikizipata huwa naomba nibadilishane na mtu anipe noti au nitanunua chochote ili tu nisikae nazo!
Nipe basii mdogo ukiwa unazipata, me nazipenda kweli kwenye usafiri wa daladala..!
 
mimi nazipendaga
ila yakizidi watu wanaogopa chuma ulete/zinawachosha kuhesabu
 
Nipe basii mdogo ukiwa unazipata, me nazipenda kweli kwenye usafiri wa daladala..!

Hahahah usijali dada, tutakuwa tunabadilishana unanipa noti nakupa hizo misarafu.

I miss you big time Sis, it’s been a while I haven’t heard from you aisee.
 
Back
Top Bottom