Shilingi Trilioni 3.554 Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 2023/2024

Shilingi Trilioni 3.554 Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 2023/2024

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

BAJETI YA TRILIONI 3.554 KUBORESHA MIUNDOMBINU NCHINI - WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI

Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imeliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha zaidi ya shilingi Trilioni 3.5 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya miundombinu ya barabara, madaraja, viwanja vya ndege, reli, meli, vivuko, majengo ya Serikali na ununuzi wa ndege.

Fedha hizo zimeombwa ili kuimarisha huduma za usafiri na usafirishaji kote nchini na hivyo kuimarisha ukuaji wa uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Akiwasilisha mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema pamoja na mambo mengine fedha hizo zinatarajiwa kujenga miradi ya kihistoria yenye urefu wa kilometa 2,035 nchini ikiwemo barabara za Kidatu - Ifakara - Lupilo - Malinyi - Kilosa kwa Mpepo - Londo - Lumecha hadi Songea KM 435.

Miradi mingine ni barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago - Maswa hadi simiyu KM 339 na barabara ya Handeni – Kibirashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboroti – Mrijochini – Dalai – Chambalo – Chemba – Kwa mtoro hadi Singida KM 460.

Aidha, Prof. Mbarawa amefafanua kuwa Serikali itaendeleza ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam – Mwanza KM 1,219 katika vipande vitano vya awamu ya kwanza ya ujenzi ili kuhakikisha vinakamilika kwa wakati na kwa thamani halisi ya fedha.

“Mheshimiwa Spika vipande hivyo ni Dar es Salaam – Morogoro KM 300, Morogoro – Makutupora KM 422, Mwanza – Isaka KM 341, Makutupora – Tabora KM 368 na Tabora – Isaka KM 165 ambavyo ujenzi wake uko katika hatua mbalimbali za utekelezaji”, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, Serikali itaendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa SGR sehemu ya Tabora – Kigoma KM 506 ambapo mkataba wake umesainiwa na kwa sasa mkandarasi anakamilisha maandalizi ya ujenzi.

Awali akitaja vipaumbele vya Sekta ya Ujenzi Prof. Mbarawa amesema ni pamoja na kuanza ujenzi wa barabara ya Express way kutoka Kibaha-Chalinze-Morogoro yenye urefu wa KM 205 kwa mfumo wa PPP na kuendeleza ujenzi wa barabara kuu zenye urefu wa KM 350 ambapo kilometa 282 zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na kilometa 68 ni miradi mipya.
 

Attachments

  • FwvRWUhWIAIIdYK.jpg
    FwvRWUhWIAIIdYK.jpg
    62.7 KB · Views: 10
Back
Top Bottom