Shillingi inazidi Kuporomoka

Najijua

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Posts
1,040
Reaction score
182
Wakuu badala ya kujadili nani kashinda na kushindwa kaytika chaguzi ndogo za UDIWANI na Nani karusha bomu uchumi wetu na shillingi yetu vinazidi kuporomoka.

Leo shilling ya Tanzania imedilishwa kwa SH 1650 dhidi ya dollar ya Marekani. Hii inashiria nini? naiona kwa mbali sasa hivi itafika sh 2,000/= kwa dollar.


Ila ndani ya nchi hii ni ruksa fedha za kigeni kulipia huduma mbali mbali kama pango katika majengo ya serikali na binafsi, ni ruksa kulipa kwa fedha za kigeni katika mahoteli, ni ruksa kulipa bandarini na TRA kwa fedha za kigeni.






Mie sio mchumi ni mbumbu wa Uchumi ila nilipata bahati ya kusoma uchumi katika semister ya mwisho nikiwa namalizia elimu yangu ya juu na kufundishwa haya ni moja ya mambo huachangia shillingi ya nchi kuporomoka.


Je, wachumi na serikali hawajui haya? hawaoni kuna haja ya kuilinda shillingi yetu na uchumi wetu? tunahitaji mwekezaji aje arekebishe uchumi? tunahitaji profesa wa kizungu atuambie ndio tuamke?
 

Napendekeza tuweke picha ya Mchumi first class MWIGULU NCHEMBA itapandisha thamani ya shilingi.
 
Ndugu yangu Janga kuu la Shilingi yetu ni wawekezaji uchwara tukio nai wano kusanya Faida kwa Shilingi na Wakitaka kuiamishia kwao inabidi wachukuwe Dilari zetu. Na mfano Mkubwa wa Hawa ni Makampuni ya simu.

Shilingi yetu haitakaa itengamae tena mpaka hapo tutakapo jitambua na kupambana na hawa wawekezaji wanaovuna Shilingi Nchini na Kutuma Dola Kama faida nchini mwao.
 
U have to understand that when the shilling looses its value,there a people who gain and the loosers!so which category do u belong?pole kama u are a looser!!!!!!!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Sina majibu kwa maswali ya muanzisha mada bali nina maswali mengi zaidi ambayo nami nayatafuta majibu. Maswali yenyewe ni kama yafuatavyo:


  1. Kwa nini Benki Kuu iliamua kutengeneza noti mpya miaka kama mitano iliyopita? (Nakumbuka Gavana alisema sababu kuu ilikuwa ni ongezeko la noti feki na hivyo kulikuwa na haja ya kutengeneza noti mpya ambazo ni madhubuti. Mwenye sababu nyingine atukumbushe)
  2. Kama ninalolikumbuka ndiyo sababu basi naleta swali jingine. Kwa nini noti za zamani bado zinatumika wakati mmoja na hizi mpya na athari yake katika Uchumi ni nini? Sijui wangapi wanafuatilia na wamegundua kuwa Benki Kuu bado inapambu noti za zamani mtaani?!
  3. Je, hii inamaanisha hizo noti za zamani baada ya kukaa kwa takribani miaka mitano kwenye sefu za B.O.T zimekuwa madhubuti kiasi cha wahaini kusahau au kuteketeza mitambo ya kuzighushi?
  4. La mwisho ni uchunguzi binafsi. Hitimisho lake unaruhusiwa kulihoji kwa kufanya utafiti wako mwenyewe. Je, wajua kuwa miongoni mwa wenye vibali maalumu vya kuagiza na kusambaza machine za kuhesabia pesa, ambazo pia husaidia kubaini noti bandia ni wale wale ambao siku zote wanashukiwa kuleta mtikisiko wa Kiuchumi kwa kutengeneza noti bandia?

Tukiweza kupata majibu ya maswali haya, tutajua kwa nini suala la kushuka kwa thamani ya shilingi na mtikisiko wa uchumi unaochangiwa na mzunguko wa noti feki haliwaumizi kabisa wanasiasa wetu, Gavana na Wachumi wa nchi hii walioko katika dola.

Nakala kwa: Mwigulu Nchemba, Nape Nnauye, HKigwangalla, Zitto
 
U have to understand that when the shilling looses its value,there a people who gain and the loosers!so which category do u belong?pole kama u are a looser!!!!!!!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Huna budi kwanza kuelewa kushuka kwa thamani ya shilingi na kudhoofika kwa shilingi (kushuka ni static na inaweza kuwa ni strategic lakini kudhoofika ni dynamic na si strategic)
Ni kweli, kushuka kwa thamani kunaweza kunawanufaisha baadhi ya watu hususan inapodhoofika lakini ni egemezi dhaifu la hoja za kiuchumi kwa sababu wafaidika ni wachache ambao ni speculators wengine ambao exporters na importers wanaumia. Exporters wanafaidika kunapokuwa na kushuka kwa thamani ya sarafu kunakoendana na uzalishaji mkubwa hivyo kuongeza uwezo wa ku-export ambao utaendelea kuchochea uwekezaji na uzalishaji hatimaye kunawiri kwa uchumi na budi kusiendane na kudhoofika kwa sarafu, (kudhoofika kupungua thamani kila uchao kama kinachotoea sasa). Kwa kuwa mauzo yetu nje ni dhaifu, kushuka kwa shilingi yetu ni matokea ya kutetereka kwa uchumi na hivyo hakuna net benefits inayopatikana kwa Taifa. Hii inachangiwa na kupungua kwa inflows na hivyo kuongezeka kwa utegemezi wetu. China anaweza kuipunguza shilingi yake na kuwa stable kwa sababu ana inflows kubwa sana ya dola na hivyo kutokuwa na utegemezi wowote wa nje kwa fedha za kigeni, zaidi yeye ndiye anayewapa fedha US(hizo dola). Katika hali kama hii, BOT huwa wanapata wakati mgumu sana kwa sababu hakuna ushirikiano kutoka sekta nyingine za uzalishaji na uagizaji hivyo wao kubakiwa na njia chache sana za kukabiliana na hali hii ikiwa pamoja na kuongeza idadi ya fedha za kiggeni sokoni, hata hivyo hili huwa linakuwa na ufanisi wa muda mfupi na kwa kuwa hakuna udhibiti wa kuingiza au kuondosha fedha za kigeni nje, njia hii inafeli na hali kurejea kuwa mbaya kuliko ile ya mwanzo. Uzalishaji?
 
First class mchumi Mwigulu Nchemba tafadhali tusaidie tafsiri ya Shillingi yetu kushuka? ni strategy ya serikali ya chama chako au bahati mbaya? Tueleze ndani ya nchi yenye sarafu yake kwanini tunaruhusu kutumika kwa fedha za nchi nyingine kufanya matumizi/manunuzi/malipo ya huduma?
 
Nashukuru kwa mada nzri.
1. Hapa tatizo c watendaji wa serilkali wala nini? Hawa watu wamesoma na wana uelewa mkubwa saana ktk economic and financial matters. Tatizo ni siasa hata ktk mambo ya kitaifa! Mfano hivi CCM imepata wapi hela za kulipa na kufungua kesi ovyo ovyo? Kwenda chinakurangua vifaa na vingine vya hatari , kuagiza gari meeengi ya kelele mjini, Green Gurd wamekuwa magaidi sn hapa mijini.
2. Kuwa na hela mbili zilizo ingizwa ktk circulation kisiasa-kwanza original zenyewe ndo fake zenyewe. Hazina sifa ya durability hata kidogo. Ni dili la watu kwa manufaa binafsi, ukikumbuka mweziwa kwanza hata mabeki mengi hapa Bongo yaliwapa wateja wao fake money!! Hivyobasi kama unabisha muulize Dr. Mgimwa Kuhusu the total notes and coins in the circulation of Tshs worldwide kama hajajikanyaga hadi asubuhi!!! Kwani hela ziko mbili na zingine ni za watu binafsitu na c za serikali. Angalia dollar ya marekani every where bt the economy isstable.
3. Nchi ni lazima ihakikishe inakua na viwandav ingi ndani ili tuongeze exports na c kuwa na imports nyingi hata za pilipili,toothpick, madishi, sabuni, etc tukaribishe wawekezaji wawekeze ndani na c kuwabingwa wa ku import hata fake products.
4. Professionalism should lead the country andnot politicians and friendship.
 
Tatizo ninaloliona mimi ni system tuliyo nayo ya 'TECHNICS KNOWS WHO INSTEAD OF TECHNICS KNOWS HOW'.

Ifikewakati watu waliosomea fani fulani wapewe kazi walioisomea lakini leo ukienda pale wizarani au pale BOT unakuta watoto na ndugu wa vigogo ndio wana sauti kubwa kuhusu mipango na uchumi na hakika hawajui lolote ila wanafanya kwa mazoea tu. Hatua za makusudi zisipochukuliwa kwa haraka, hakika iko siku tutapishana na shilingi ya Uganda, wao wakipanda nasi tukishuka tena kwa kasi ya ajabu. Watanzania sijui nani katuloga......!
 
kwanza kabisa kila mtu ajitume kufanya kazi ,kimsingi watz wanajituma sana ila wanaangushwa na watu waliopewa dhamana ya kuliongoza taifa na wasimamiji wa sera ikiwa ni pamoja na sera za uchumi...unategemea nini kama line ya simu inaanza kulipiwa ilhali madini (wageni) hawatozwi kodi .hii nchi yangu inanifanya nisione fahari ya kuwa mtz tunathamini wakoloni(wawekezaji) zaidi ya wananchi(wazawa)
 
Shilingi inasimamiwa na Mtalii kutwa ni kudhurura na kuchekacheka mpaka 2015 hatokuwa na thamani kabisa
 

Pamoja na mapambo ya maelezo kedekede ya wataalamu wa uchumi kutueleza sababu za kushuka au kupanda thamani pesa, kwangu mimi naona kwa Tanzania uzoefu wangu ni tofauti na maelezo yao kabisa.

Kipindi cha uongozi wa Nyerere tulishuhudia pesa kushuka thamani kwa kiwango kidogo mno, na sababu kubwa Nyerere hakuwa na hulka ya kujenga uchumi tegemezi wa kuombaomba huku na kule. Alitumia rasilimali na mapato ya humu humu nchini, ingawa kulikuwa na miradi kadhaa ya maendeleo iliyofadhiliwa hasa na nchi za China na Japan, hata hivyo ilikuwa ni kwa kiwango kidogo.

Kipindi cha Mzee Ruksa mfumuko wa bei ulianza kuinuka zaidi na inaeleweka kwa sababu ya sera za mfumo wa uchumi wa biashara huria na utandawazi alipofungua mapazia kuruhusu hewa mpya iingine na watu kuanza kujigonga vichwa vyao kwenye vioo kushangaa vitu vinavyozidi kumiminika madukani. Hata hivyo deni lilionekana kuongezeka kipindi Cha Mzee Ruksa sababu siwezi kujua kwa ndani maana muda huo mambo ya serikali yalikuwa ya siri kali huko Mkulu na baraza lake la mawazini, na Mrema alipotaka kuhoji basi alipata kichapo na kusukumiwa nje ya uringo kwa sababu alikuwa anarusha ngumi isivyokubaliwa na mwamuzi wa pambano.

Nzee Nkapa alipoingia madarakani, alishtushwa na deni kubwa la Taifa na hivyo kufanya diplomasia na mataifa yale yanayotudai kushawishi yatupe unafuu kwa kufuta, na alifanikiwa mataifa mengi yalifanya hivyo. Nzee Nkapa akaanza namna yake ya kujenga uchumi wa kujitegemea kwa kuanza miradi ambayo chanzo cha mapato kilikuwa hapa hapa nyumbani kama bomba la maji toka ziwa Viktoria, na ujenzi wa Daraja kwenye mto ruvuma kuunganisha Msumbiji na Tanzania.

Alipoingia Vasco da Gama
aka Faster Jet ni kama mtu mwenye mapepo vile, maana pale Ikulu hapakaliki sijui kuna mapepo yanamsukumia nje? Ni kurukaruka huku na kule kutembeza bakuli hata yule hayati ombaomba wa Dodoma hafui dafu. Obama amemwonya kiaina aliposema Afrika itajengwa na waafrika wenyewe, lakini sijui Kama Faster Jet alimwelewa, alibaki kuchekacheka tu na kuwashangaa wazungu walioongozana na Obama kana kwamba hakuwahi kuwaona na kuwavutia wamtazame usoni anapochekacheka.

Uchumi 75% tegemezi tautazamie nini?
Deni la taifa limepaa isivyo kawaida tangu nchi hii ipate uhuru haijatokea. Deni hilo ni kutokana na kupitisha bakuli huku na huko kila kukicha na anachokinga kwenye bakuli hatukioni huku akitumia mabililioni kuruka huku na huko na anachoambalia aendako hakijai kwenye kiganja huku akiwavutia kuja kusomba rasilimali za taifa letu ambazo ndizo zingetumika ilivyo ndizo zingepandisha dau la thamani ya pesa yetu.

Thamani ya Pesa itazidi kuporomoja tu kwa mtindo wa kutegemea maisha ya kuombaomba tofauti na nchi ambazo zimesimama kwa uchumi wa kujitegemea.
 

Kama hutamindi nitaongezea hapo swali la tano.

Kwa nini Benki Kuu ilimwaga midola sokoni alipokuja Obama?

Au labda kuja kwa Obama kulifanya shilingi ipande bei fasta?
 
yeye mwenyewe Vasco Da Gama alita shilingi yetu hela ya madafu,sasa kaam hajivunii shilingi yeto u ategemea atakuwa na uchungu nayo,tukubali tu kwamba tuliiingiza chaka kumpa nchi huyu jamaa,kuna watu walisema ati jamaa ni handsome hata kwenye hela akiweka picha yake itapendeza.....mweee!UOTE=Candid Scope;6778817]Pamoja na mapambo ya maelezo kedekede ya wataalamu wa uchumi kutueleza sababu za kushuka au kupanda thamani pesa, kwangu mimi naona kwa Tanzania uzoefu wangu ni tofauti na maelezo yao kabisa.

Kipindi cha uongozi wa Nyerere tulishuhudia pesa kushuka thamani kwa kiwango kidogo mno, na sababu kubwa Nyerere hakuwa na hulka ya kujenga uchumi tegemezi wa kuombaomba huku na kule. Alitumia rasilimali na mapato ya humu humu nchini, ingawa kulikuwa na miradi kadhaa ya maendeleo iliyofadhiliwa hasa na nchi za China na Japan, hata hivyo ilikuwa ni kwa kiwango kidogo.

Kipindi cha Mzee Ruksa mfumuko wa bei ulianza kuinuka zaidi na inaeleweka kwa sababu ya sera za mfumo wa uchumi wa biashara huria na utandawazi alipofungua mapazia kuruhusu hewa mpya iingine na watu kuanza kujigonga vichwa vyao kwenye vioo kushangaa vitu vinavyozidi kumiminika madukani. Hata hivyo deni lilionekana kuongezeka kipindi Cha Mzee Ruksa sababu siwezi kujua kwa ndani maana muda huo mambo ya serikali yalikuwa ya siri kali huko Mkulu na baraza lake la mawazini, na Mrema alipotaka kuhoji basi alipata kichapo na kusukumiwa nje ya uringo kwa sababu alikuwa anarusha ngumi isivyokubaliwa na mwamuzi wa pambano.

Nzee Nkapa alipoingia madarakani, alishtushwa na deni kubwa la Taifa na hivyo kufanya diplomasia na mataifa yale yanayotudai kushawishi yatupe unafuu kwa kufuta, na alifanikiwa mataifa mengi yalifanya hivyo. Nzee Nkapa akaanza namna yake ya kujenga uchumi wa kujitegemea kwa kuanza miradi ambayo chanzo cha mapato kilikuwa hapa hapa nyumbani kama bomba la maji toka ziwa Viktoria, na ujenzi wa Daraja kwenye mto ruvuma kuunganisha Msumbiji na Tanzania.

Alipoingia Vasco da Gama
akaFaster Jet ni kama mtu mwenye mapepo vile, maana pale Ikulu hapakaliki sijui kuna mapepo yanamsukumia nje? Ni kurukaruka huku na kule kutembeza bakuli hata yule hayati ombaomba wa Dodoma hafui dafu. Obama amemwonya kiaina aliposema Afrika itajengwa na waafrika wenyewe, lakini sijui Kama Faster Jet alimwelewa, alibaki kuchekacheka tu na kuwashangaa wazungu walioongozana na Obama kana kwamba hakuwahi kuwaona na kuwavutia wamtazame usoni anapochekacheka.

Uchumi 75% tegemezi tautazamie nini?
Deni la taifa limepaa isivyo kawaida tangu nchi hii ipate uhuru haijatokea. Deni hilo ni kutokana na kupitisha bakuli huku na huko kila kukicha na anachokinga kwenye bakuli hatukioni huku akitumia mabililioni kuruka huku na huko na anachoambalia aendako hakijai kwenye kiganja huku akiwavutia kuja kusomba rasilimali za taifa letu ambazo ndizo zingetumika ilivyo ndizo zingepandisha dau la thamani ya pesa yetu.

Thamani ya Pesa itazidi kuporomoja tu kwa mtindo wa kutegemea maisha ya kuombaomba tofauti na nchi ambazo zimesimama kwa uchumi wa kujitegemea.
[/QUOTE]
 
yeye mwenyewe Vasco Da Gama alita shilingi yetu hela ya madafu,sasa kaam hajivunii shilingi yeto u ategemea atakuwa na uchungu nayo,tukubali tu kwamba tuliiingiza chaka kumpa nchi huyu jamaa,kuna watu walisema ati jamaa ni handsome hata kwenye hela akiweka picha yake itapendeza.....mweee
 
tukizuia matumizi ya dola katika uchumi wetu basi kwa kiasi fulani tutaongeza thamani ya shilling, mfano ukienda maduka mengi au sehemu nying kwa sasa wanatumia dollar kama njia ya malipo kitu ambacho sio sawa kwenye uchumi wako.
 

Hata hili la kuruhusu kuuza na kununua dola kama karanga linachangaia sana kuididimiza shilingi yetu dhidi dola, hamshangai hadi Wazairi Lukuvi akatamka Bungeni shilingi ni pesa za madafu! Wakubwa wana maslahi binafsi ktk biashara za maduka ya Bureau de Change na kwa kiasi kikubwa zinatumika kutorosha dola kutoka nchini maana hakuna udhibiti ktk biashara hiyo. Tujiulize, kwa nini ni rahisi sana kununua shilingi ktk maduka ya Bureau de Change kuliko kununua dola? Ukienda kuuza dola hakuna maswali, lkn ukienda kununua dola mikwara inakuwa mingi!
 
shilling lazima ishuke sababu tunaagiza sana kuliko kuuza nje.
pia ata hotel za kifahari mfano za serengeti zinamilikiwa na matajiri wa kigen hivo uweka pesa yao nje ya tanzania.
inapelekea kukosa pesa za kigeni hivo lazima shilling ishuke.
hii ni inevitable yani aiepukii adi tuuze sana nje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…