Najijua
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 1,040
- 182
Wakuu badala ya kujadili nani kashinda na kushindwa kaytika chaguzi ndogo za UDIWANI na Nani karusha bomu uchumi wetu na shillingi yetu vinazidi kuporomoka.
Leo shilling ya Tanzania imedilishwa kwa SH 1650 dhidi ya dollar ya Marekani. Hii inashiria nini? naiona kwa mbali sasa hivi itafika sh 2,000/= kwa dollar.
Ila ndani ya nchi hii ni ruksa fedha za kigeni kulipia huduma mbali mbali kama pango katika majengo ya serikali na binafsi, ni ruksa kulipa kwa fedha za kigeni katika mahoteli, ni ruksa kulipa bandarini na TRA kwa fedha za kigeni.
Mie sio mchumi ni mbumbu wa Uchumi ila nilipata bahati ya kusoma uchumi katika semister ya mwisho nikiwa namalizia elimu yangu ya juu na kufundishwa haya ni moja ya mambo huachangia shillingi ya nchi kuporomoka.
Je, wachumi na serikali hawajui haya? hawaoni kuna haja ya kuilinda shillingi yetu na uchumi wetu? tunahitaji mwekezaji aje arekebishe uchumi? tunahitaji profesa wa kizungu atuambie ndio tuamke?

Sina majibu kwa maswali ya muanzisha mada bali nina maswali mengi zaidi ambayo nami nayatafuta majibu. Maswali yenyewe ni kama yafuatavyo:
- Kwa nini Benki Kuu iliamua kutengeneza noti mpya miaka kama mitano iliyopita? (Nakumbuka Gavana alisema sababu kuu ilikuwa ni ongezeko la noti feki na hivyo kulikuwa na haja ya kutengeneza noti mpya ambazo ni madhubuti. Mwenye sababu nyingine atukumbushe)
- Kama ninalolikumbuka ndiyo sababu basi naleta swali jingine. Kwa nini noti za zamani bado zinatumika wakati mmoja na hizi mpya na athari yake katika Uchumi ni nini? Sijui wangapi wanafuatilia na wamegundua kuwa Benki Kuu bado inapambu noti za zamani mtaani?!
- Je, hii inamaanisha hizo noti za zamani baada ya kukaa kwa takribani miaka mitano kwenye sefu za B.O.T zimekuwa madhubuti kiasi cha wahaini kusahau au kuteketeza mitambo ya kuzighushi?
- La mwisho ni uchunguzi binafsi. Hitimisho lake unaruhusiwa kulihoji kwa kufanya utafiti wako mwenyewe. Je, wajua kuwa miongoni mwa wenye vibali maalumu vya kuagiza na kusambaza machine za kuhesabia pesa, ambazo pia husaidia kubaini noti bandia ni wale wale ambao siku zote wanashukiwa kuleta mtikisiko wa Kiuchumi kwa kutengeneza noti bandia?
Tukiweza kupata majibu ya maswali haya, tutajua kwa nini suala la kushuka kwa thamani ya shilingi na mtikisiko wa uchumi unaochangiwa na mzunguko wa noti feki haliwaumizi kabisa wanasiasa wetu, Gavana na Wachumi wa nchi hii walioko katika dola.
Nakala kwa: Mwigulu Nchemba, Nape Nnauye, HKigwangalla, Zitto