Asante mkuu kwa mchango wako.
Sasa kushuka kwa thamani ya Shillingi kuna uhusiano gani na mfumuko wa bei? Najua ukienda kwenye maduka mengi sasa hivi naq hasa yanayouza vitu amabavyo ni imported unakuta vitu vimepanda bei ukiwauliza wanakwambia bei ya dola imepanda hivyo wanalazimika kuongeza bei ili wapate thamani halisi ya pesa walizotumia kununua hizo bidhaa. Je ili lina ukweli wowote au watu wanajaribu kutumia nafasi hiyo kutengeneza super profit? Je kushuka thamani kwa shilingi kutakuwa na athari gani kwenye bei ya mafuta locally?
Tiba
Tiba,
Sarafu ya nchi ina thamani kutoka na mahitaji ya kutumika sarafu husika nchini. Kwahivyo, kama sarafu ya nchi ikiwa haihina mahitaji thamani ya sarafu hushuka. Quantity theory money inasema thamani ya sarafu inasababishwa na vitu viwili kwanza mfumuko wa bei nchi na kiwango cha sarafu katika mzunguko wa pesa. Tanzania shilling inashuka kutokana na kukosekana na mahitaji ya sarafu nchini, mfumuko wa bei na ufisadi.
A. Kukosekana kwa mahitaji ya sarafu nchini:
Kusema ule ukweli hili swala serikali inaonekana either imelinyamazia kimya au kuna vigogo wanafaidika nalo (hasa kwenye sekta ya nyumba mfano Dar wapangishaji hudai dollar kama malipo ya pango, au baadhi ya shule Dar nazo pia hudai ada kwa dollar). Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya sarafu ya nje nchini sarafu ya tanzania inashuka thamani. Hilo linachangia kwa kiwango kikubwa kukuwa kwa mahitaji ya sarafu za nje nchini na pia kushuka kwa thamani ya Tanzanian shillings. Ukiatazama volatility ya currency (mtiririko wa sarafu) utanyambua kwamba sarafu yetu haina stability kwani ikishuka dollar nayo inashuka, dollar ikiwa strong nayo inakuwa strong na hivyo basi utaona kuwa sarafu yetu haina thamani kama mtoto yatima inaenda popote sarafu ya kimataifa inapoelekea.
B. Mfumuko wa bei:
Mfumuko wa bei wa nchi yetu unachangiwa na mambo mawili, cost push inflation inayotokana na mfumuko wa bei ya mafuta duniani, European sovereign debt crisis, na maumivu ya mtikisiko wa sekta ya benki. Mfumuko wa bei ya mafuta duniani unaosababishwa na speculators (kwasababu Financial Times- April walitamka wazi bei halisi ya mafuta Crude Brent Oil haizidi hata $70 kwa pipa) ambao wanaipaisha bei ya mafuta kutokana na machafuko ya mashariki ya mbali (middle east). Machafuko haya hao speculators huwa wanacheza kamari ya kubadilishana bidhaa wakihofia machafuko hayo yanaweza kusababisha uhaba wa mafuta katika soko la dunia. Mategemeo ya nchi za kimagharibi yameanza kufifia kwani walitegemea hali ya amani itarejea mashariki ya mbali lakini bado haijawa shwari hasa Libya. Ndio ya kwamba International Energy Agency (IEA) walifungua reserves zao kujaribu kushusha bei ya mafuta (kwa lengo hasa kuwafaidisha marekani kwani siku za mapumziko ziko mbeleni). Pia uamuzi wa kufungua mafuta ya akiba ulikuja baada ya nchi za Opec kushindwa kufikia muafaka wa kuongeza uzalishaji wa mafuta katika soko la dunia (OPEC). Kwa ufupi bei ya mafuta imeanza kushuka kwa kasi sasa ila wanauchumi hawategemei itadumu kwani mahitaji ya mafuta yako palepale. Mfumuko wa bei ya mafuta umechangia kwa kiwango kikubwa mfumuko wa bei nchini na kufanya maisha ya watanzania kuwa bei ya juu.
Pia mfumuko wa bei umesababishwa pia kwa kukua kwa gharama za uzalishaji nchini kutokana na kukosekana na nishati ya umeme nchini. waziri wa nishati wakati akicheza makida makida gharama za uzalishaji zimekuwa zikiongezeka kuchangia mfumuko wa bei kwa kiwango kikubwa. Jambo hili linaweza kutatulika kama utapatikana umeme wa uhakika nchini.
Pia mfumuko wa bei umechangiwa na kuongezeka kwa purchasing power ya watanzania (demand pull). Serikali ya mkapa walijitahidi na kufanikiwa kupunguza mfumuko wa bei unaotokana na demand pull. Kama umerudia kumbukumbu zako mishahara ya mtanzania wakati wa mkapa ilikuwa haipandi ovyo na hivyo kusaidia kwa kiwango cha aina fulani kushuka kwa kasi ya mfumuko wa bei. Serikali ya Kikwete imekuwa ikiongeza mishahara kila kukicha na kuchangia kuongezeka kwa kiwango cha purchasing power ya mtanzania. Hivyo basi, kumeongeza gharama za maisha ya kufumua mfumuko wa bei nchini. Kuongezeka kwa gharama za uzalishaji, uwezo wa mtanzania kununua kumechangia kukuza mfumuko wa bei na hivyo kusababisha thamani ya shillingi kuporomoka.
Mtikisiko wa madeni ya nchi hasa kwa nchi za ulaya pia umechangia kuwapo na mabadiliko yasitabirika ya sarafu katika ulimwengu (Volatility). Hilo linatokana na hofu ya kuvunjika kwa Umoja wa nchi za ulaya, contagion effect ya greece hasa kwa nchi za spain, Italy, Ireland na Portugal. Pia debt risk exposure kwa benki za US, UK na Hongo Kong na China. Kutokana na hilo utagundua sarafu za Asia zimekuwa zikipanda thamani sana kuliko za ulaya kutoka na wasiwasi uliopo sasa hasa kutokana na kile kinachoendelea Ugiriki na Ulaya nzima. Kwetu hatujasalimika kwani sarafu yetu imeunganishwa na US dollar (currency peg) na basi utagundua sarafu yetu leo imeamka hivi kesho imeamka vile.
Pia kuporomoka kwa sekta ya viwanda na kupungua kwa mauzo ya bidhaa za kilimo nje ya nchi na kudorora kwa bei za malighafi za kilimo kama katani, kahawa nk. kumechangia kwa kiwango kikubwa kuwapo kwa uhaba wa sarafu nchini. Sekta ya viwanda imekufa kabisa kiasi kwamba nchi yetu imekuwa ikitegemea bidhaa za nje badala za nchini hadi vyakula na kupelekea kuwapo na mfumuko wa bei nchini. na uhaba sarafu za kigeni.
C. Ufisadi:
Ufisadi una mchango wa kiasi kikubwa kuporomoka kwa sarafu nchini. Niliwahi kusema nyuma kwamba ukitaka kujua thamani sarafu imeshuka kwa kiasi kikubwa chukua taarifa za sarafu BOT (Refer to their website). Ukiziweka katika Excel ukatengeneza graph utaona trend ya thamani ya shillingi iliporomoka kwa kiasi kikubwa miaka ya 2005-2006. Miaka hii ndio majanga ya ufisadi kama EPA yaliitikisa nchi, BOT twin tower, na madudu mengineyo. Hii trend ya kuporomoka sarafu ya nchi miaka hii wakati kulikuwa hakuna mtikisiko wa kiuchumi duniani wala mfumuko wa bei ya mafuta unapelekea kupata jibu moja la kwamba sarafu ya nchi thamani yake ilikuwa inaporomoka kutokana na watu kuwa wananunua dollar, pound kwa kiwango kikubwa ili either wasafirishe nje ya nchi (capital flight). Waliokuwa wakifanya ufisadi walikuwa either wakinunua dollar kwa wingi nchini au wakizisafirisha kwa kutumia njia ya fedha nje ya nchi.
BOT inafanya nini?
Binafsi naona BOT hawana wanalolifanya kuokoa shillingi kwasababu kwa tamko la Benno ndulu (nimekata tamaa kumuita professor ameniangusha sana) naona wamekuwa wanajaribu kutafuta sababu za kuhalalisha sarafu kwanini inashuka badala ya kushukulikia hilo jambo.
Nini kifanyike:
A. Ununuzi wa dhahabu:
Namuunga mkono Zitto kabwe pendekezo lake la kununua dhahabu kwani katika soko la sasa na matatizo ya madeni. bei ya dhahabu imekuwa ikipanda mno. Hili jambo litachangia kuifanya sarafu iwe na thamani kwani italinganishwa na kiwango cha dhahabu nchi inayo katika reserves. Ni vema BOT wapunguze reserve za dollar kwani dollar inashuka thamani na forecast zinaonyesha uchumi wa marekani haukui ilivyokuwa inategemewa. Pia matatizo ya madeni ya nchi yamesababisha kushuka thamani za sarafu ya Euro na sterling pound. Ni vema tupunguze ukubwa reserves za foreign currencies na kuongeza kiwango cha dhahabu nchini.
b. Kupunguza matumizi ya foreign currency nchini:
Dollarisation inabidi kutomezwa venginevyo thamani ya shillingi nchini itaendelea kuporomoka.
c. Kutokomeza ufisadi:
Kutasaidia kupunguza mahitaji ya fedha za kigeni na kupelekea sarafu yetu kuimarika.
d. Tax reduction:
Kupunguza kodi katika sekta ya mafuta kutapunguza mfumuko wa bei na kupunguza gharama za uzalishaji.
e. Umeme wa uhakika utasaidia kuongeza uhai wa sarafu na kupunguza gharama za maisha nchini.
f. Kujaribu kutokuongeza mshahara badala yake wapunguze kodi ya makato ya mshahara. Hilo litasaidia kupunguza purchasing power ya mtanzania nchini.
Natumai nimekufunua kidogo Mkuu.
Nilikuwapo!!!