Shilole aamua kumtafuta 'Ticha' wa Kumfundisha Kimombo

Shilole aamua kumtafuta 'Ticha' wa Kumfundisha Kimombo

Ila shilole hua anajiamini hua ananipa raha sana
 
Hajui kingereza kweli
Ila anazuga kujiongeresha broken ili tujue anatuzuga tuu
Kumbe kingereza kwake shubiri.
 
Huyu dada hajasoma ila anapenda kujua kiingereza na anajikubali hajui ila anataman kujua, vzuri
 
Mwisho wa siku atakielewa kuliko wewe mwenye aibu katika kujifunza na itabaki story tu mara ooh kajifunza juzijuzi tu hapa
 
Hyu ni binti anayetaka kujiendeleza ana confidence atafika mbali. Anawakumbusha tu vijana wenzane wasiojua kiingereza halafu wana pesa basi watafute mwalimu awafundishie nyumbani maana kwenda kwenye shule hizi wanaona aibu. Kitu nachoweza kusema atafika mbali as anajua tatizo lake. Anajua kazi yake akijua kiingereza itampaisha Zaidi. Congratulations Shilole utafanikiwa!
 
View attachment 366044
Msanii Shilole amesema ameamua kumtafuta mwalimu wa kumfundisha lugha ya Kiingereza inayompa shida kuwasiliana na watu mbalimbali.

‘’Ni kweli nataka nifundishwe vizuri najua kidogo tu vya kuungaunga ‘sometimes Yes sometimes No’ nataka kwenda mbali zaidi, nataka nisome kwa furaha zangu lakini sio kwenda chuo, wanaoenda chuo hawana hela mimi hela ninazo, unajua watu wanenda kusoma ‘english coz’ ili wapate hela mimi nasoma tu ili nikikutana na akina Beyonce nisipate shida nitasoma kwa mwezi mmoja kwa sababu kichwa change kiko vizuri’’ alisema Shilole.





mzungu mzungukeni
 
Back
Top Bottom