Shilole afunguka kuhusu kupigana na mumewe

Shilole afunguka kuhusu kupigana na mumewe

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Msanii wa muziki nchini Tanzania, Zuwena Mohamed 'Shilole' amesema hawezi kuthubutu kwa sasa kupigana na mume wake Uchebe kwa kwa madai amekuwa na mapenzi ya kupigana yalikuwa ya utoto.

Shilole amebainisha hayo kupitia eNewz inayorushwa na EATV baada ya kuzoeleka na watu wengi kwa tabia yake ya kupiga wanaume ambao anakuwa nao katika mahusiano na kusema kwa sasa hawezi kuthubutu kufanya hivyo na kama atampiga mume wake basi ni wakiwa faragha nasio pengine.

Shilole.jpg

"Mume wangu ni mwanaume mwenye msimamo katika jambo lake ambalo anataka kulifanya. Siwezi kupigana nae maana alikuwa anapigana kabla ya kuwa nami na ana mkanda huyo usimuone hivyo. Mambo ya kupigana yalikuwa zamani ya kitoto lakini sasa hivi nimekuwa siwezi kusema nataka kupigana na mume wangu wala mume wangu hawezi kusema ainue mkono anipige", amesema Shilole.

Pamoja na hayo, Shilole ameendelea kwa kusema "mimi ni mtu makini sana ninaejitambua na kujithamini, endeleeni kufuatilia harakati zangu ambazo ninazifanya katika haya maisha.
 
Hayo ma mama masanii watazeeka wakiwa wanaoa tuu na kutema. Kesho tuu utasikia kamfukuza na matarumbeta na mchiriku utapita tena mjini eti "anameremetaaaaaa!!!! kumbe kaoa tena!!!!!
 
Nimependa hapo kuwa "kama nitampiga basi tukiwa faragha na si hadharani"..,
 
Uchwebe iko siku yako kaa tayar Nuh alishanyolewa...
 
Back
Top Bottom