malenga wetu
JF-Expert Member
- Jan 31, 2013
- 283
- 198
Msaanii wa muzuki wa kizazi kipya (Bongo fleva) Shilole bado ana nia ya kugombea ubunge kwenye jimbo lake la Igunga, lakini anahofia maisha yake kuwa hatarini! Shilole anasema amekuwa amepokea simu nyingi kutoka Igunga zinazomtaka ajitose kuwania nafasi hiyo, lakini bado yupo njia panda.
"Unajua siasa ni ngumu mimi bado nipo kwenye mjadala wa kugombea na hii ni baada ya kuona watu wanataka kuongozwa, lakini bado nafikiria," amesema. "Nikiwa tayari nitagombea kupitia CCM. Kitu ambacho kinaniogopesha kiukweli ukiangaliwa watu waliopita ni vijana tu wanakufa mapema kutokana na mambo ya siasa. Siasa inahitaji moyo sana mimi ni muoga sana, naogopa kufa watu wanauwana! Mtu unatamani lakini ndo hivyo," ameongeza.
"Mimi napigiwa simu nyumbani Igunga, watu wengi sana kila mmoja ananiambia ‘tunakuhitaji ugombee yaani baada ya Rostam wananihitaji mimi! Mimi bado nipo njia panda mpaka sasa hivi lakini muda ukifika kila kitu mtasikia."
My Take:
Ina maana Shilole hajui kama baada ya Rostam kuna Kafumu? Ina maana hamjui hata mbunge wake!!!