Mlavumbi wa Ukweli
Member
- Jan 22, 2014
- 65
- 38
Habari zinadai kwamba baadhi ya ndugu wa msanii wa Bongo Fleva , Nuh Mziwanda ambao ni wakwe wa staa wa muziki na filamu za Kibongo, Zuwena Mohamed Shilole hawamtaki kwa madai kuwa ana umri mkubwa kuliko ndugu yao.
Baadhi ya wanandugu hao ( majina yanahifadhiwa) walisema umri wa Shilole siyo wa kuishi na ndugu yao, Mziwanda kwani hawaendani.
Ukweli ni kwamba mapenzi hayaingiliwi lakini tunaumia kuona ndugu yetu katika penzi zito na Shilole ambaye hawaendani kiumri , alidai mmoja wa ndugu hao.
Alipotafutwa Shilole ili kufikishiwa ujumbe wa ndugu hao kwamba hawamtaki , simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.
Hao ndugu wakalale
Wafate yao
hainaga kuuliza umri ile makitu!!!!
Mi ningekuwa mzazi maamuzi namwachia tu mwanangu ili mradi kafikisha umri wa kuoa na ni mtu mzima akafie mbele huko yeye mwenyewe
Wakaache kale katoto kapewe twisheni na waliokubuhu hao watoto wenzie watamsumbua kwanza ni sunna kuona aliekuzidi umri.
Age ain't nothing but a number!
Si haramu nzi kufia kwenye kidonda...kama dogo ana zaidi ya miaka kumi na nane aachwe afuate moyo wake jamani.
Kipendacho roho hula nyama mbichi...na mtoto akililia wembe mpeni.
Well said wakuu.