DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Msanii Zuena Mohamed ( Shilole ) ambaye ni Mwanzilishi na Mmiliki wa Migahawa ya SHISHI FOOD, leo Disemba 18,2025 akiwa katika eneo la Mgahawa wake wa Dar es salaam ambao ulichomwa moto katika vurugu za uchaguzi October 29, amesema amewasamehe Watu wote waliohusika kuchoma Mgahawa wake.
Akiongea na Waandishi wa Habari leo, Shilole amesema kwa sasa ameamua kutumia njia ya kufanya Delivery kama alivyokuwa akifanya hapo awali wakati anaanza biashara hiyo ya chakula ili kuifufua tena biashara yake hii ambayo anasema imewakosesha ajira Vijana takriban 200.