Shime Watanzania tuupiganie Uhuru wetu unaoporwa. Tutajuta!

Shime Watanzania tuupiganie Uhuru wetu unaoporwa. Tutajuta!

Tukija kushtuka kumekucha. Jamaa anajiona bingwa sababu ya umbumbumbu,uwoga na ubinafsi.Hata wana ccm wananung'unika ila hofu ya "njaa,kisasi" inawatafuna.UNAFIKI KWA KWENDA MBELE!
 
Mwalimu Nyerere na wenzake walipambana na mkoloni siyo kwasababu walitaka nchi yetu ipate ama ijenge vitu la hasha..
Hata wakoloni tungewaacha wangekuwa wameshatuletea maendeleo Kama barabara,majumba mashule n.k,,,,,,,tuliwaondoa wakoloni ili tupate UHURU.Nini maana ya uhuru?

Ni khali ya kuwa huru hata Kama ni maskini wa vitu au mawazo.Kumbe;Kama nchi zote za Afrika ziliwafukuza wakoloni,basi zilikuwa tayari kuwa maskini wa vitu ili tu ziwe HURU.
 
Hata huyo Nyerere unayemsifu hapa haujui tu ni jinsi gani alikuwa MWOVU kuliko unavyodhani.

Yeye ndiye chanzo cha udikteta na mifumo mingi mibaya kwenye hii nchi.

Waliomfuata walikopi na kupesti tu.
 
Mwalimu Nyerere na wenzake walipambana na mkoloni siyo kwasababu walitaka nchi yetu ipate ama ijenge vitu la hasha.

Mwalimu Nyerere na wenzake walipambana na mkoloni siyo kwasabb walitaka kuunda serikali itakayo watisha watu na kuwafanya wawe na "heshima" kwa watawala.

Mwalimu Nyerere na wenzake walipambana na mkoloni siyo kwasabb walitaka kuendeleza/kujenga maeneo walikotoka na kuyafanya ya kimkakati.

Akina Mwalimu Nyerere na wenzake hawakupambana na mkoloni ili wageuke chui wa kuwakamata kila atakayejaribu kutoa mawazo kinzani.

Nini waliktaka akina Mwalimu Nyerere na wenzake?

Walipambana na mkoloni ili wananchi wa nchi hii wapate UHURU wa kufanya , kusema na kutenda bila ya woga ili mradi wasitoke nje ya mipaka ya kikatiba.

Lakini sasa Uhuru hakuna tena. Katiba haiheshimiwi, watu wanatishwa, tunalingishiwa ujenzi wa miundombinu eti ndiyo kitu mihimu kuliko uhuru wetu. Ebo!

Rais bila soni anatumia mabilioni ya shilingi kujenga miundombinu mikubwa kijijini kwao. Tumenyamaza! Hakuna anayethubutu kukemea.

Amevuruga uchaguzi serikali za mitaa watanzania kimyaa! Amevuruga uchaguzi mkuu tunamwagalia tu'. Na sasa kuna kila dalili na mikakati ya wazi imewekwa ili kumuongezea muda afie madarakani. Hatusemi.

Hakika tutavuna mabua, maana tunacheka na nyani.

Namkumbuka Tundu Lisu alliyepata kuona mbali ingali bado na mapema (2016) alisema "Tuna rais wa ajabu haijapata kutokea"
Naaam, tunacheka na nyani.....
 
Back
Top Bottom