Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Watu 3 wanadaiwa kufariki na wengine 34 wakijeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Classic lililokuwa likitokea Kampala kuelekea Dar kupata ajali eneo la Buyubi Shinyanga.
Baadhi ya majeruhi kwenye ajali hiyo wamesema kuwa dereva wa basi hilo alishindwa kuimudu kona ya Didia.
Watu watatu wanahofiwa kufa katika ajali ya basi la Classic eneo la Buyubi Kata ya Didia mkoani Shinyanga, huku wengine 34 wakijeruhiwa baada ya basi hilo kuacha njia na kupinduka majira ya saa 10:00 alfajiri ya Juni 2, 2021, wakati likitokea Kampala Uganda kuelekea Dar es Salaam.
Basi la kampuni ya Classic lililopata ajali
Baadhi ya majeruhi wa ajili hao wamesema kuwa ajali hiyo imetokea baada ya dereva wa basi hilo kushindwa kukata kona katika barabara ya Shinyanga Kahama na kwamba mara baada ya ajali hiyo dereva alikimbia.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa wilaya ya Shinyanga John Kafumu, amefika eneo la tukio na kueleza kuwa taarifa zaidi kuhusiana na ajali hiyo zitatolewa na Kamanda wa Polisi mkoa Debora Magiligimba.