Shinyanga: Kituo cha Afya chagundulika kuhifadhi Damu kwenye Majokofu ya nyumbani

Mkurugenzi wa huduma za afya ustawi wa jamii na lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt.Rashid Mfaume amebaini ukiukwaji wa manunuzi ya vifaa ikiwamo jokofu za kuhifadhia damu katika kituo cha afya Mwalugulu, katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Dkt. Mfaume amebaini hayo wakati wa kukagua shughuli za uendeshaji na usimamizi wa afya katika kituo hicho akiwa ameambatana na timu ya afya, ustawi wa jamii na lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI ambapo majokofu mawili yaliyonunuliwa katika kituo hicho kwa ajili ya kuhifadhi damu yakabainika kuwa ya matumizi ya nyumbani.

“Ni majokofu kwa ajili ya kufungia nyanya,karoti na parachichi na wataalamu wametuthibitishia kuwa haya sio majokofu ya damu, huyu mzabuni tumemlipa bila kukagua tumeagiza majokofu ya kutunzia damu tumeletewa majokofu ya matunda” Amesema Dkt. Mfaume.

Kufuatia hatua hiyo Dkt. Mfaume ameelekeza mfamasia wa halmashauri kuondolewa kwenye nafasi yake kwa kutoa taarifa ya uongo wakati wa ukaguzi wa vifaa huku akielekeza kuonywa kwa maandishi kwa wajumbe wa timu ya usimamizi wa shughuli za Afya ya Halmashauri (CHMT) ya Msalala.

JAMBO TV
Ubinadamu umeisha kwa wengine
 
Tunawapongeza hao Watumishi Kwa kujiongeza.Wanaolaumu walipeleka majokofu yanayohitajika?
Unahisi hayo majokofu wamenunua wao kwa utashi wao na pesa kutoka mfukoni? Au ni fungu la serikali kwa ajili ya manunuzi wao wakapiga cha juu wakachukua friji za kueka juice ya nyumbani
 
Eeeehhh jamani, adhabu hapo inafaa iwe kali kabisa
 
Hawakujingeza, ni uzembe tu. Rudia kusoma vizuri:

“Ni majokofu kwa ajili ya kufungia nyanya,karoti na parachichi na wataalamu wametuthibitishia kuwa haya sio majokofu ya damu, huyu mzabuni tumemlipa bila kukagua tumeagiza majokofu ya kutunzia damu tumeletewa majokofu ya matunda” Amesema Dkt. Mfaume.
Wamemlipa bila kukagua! Na bado aliyelipa hachukuliwi hatua yoyote
 
Mkurugenzi wa huduma za afya ustawi wa jamii na lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt.Rashid Mfaume amebaini ukiukwaji wa manunuzi ya vifaa ikiwamo jokofu za kuhifadhia damu katika kituo cha afya Mwalugulu, katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Dkt. Mfaume amebaini hayo wakati wa kukagua shughuli za uendeshaji na usimamizi wa afya katika kituo hicho akiwa ameambatana na timu ya afya, ustawi wa jamii na lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI ambapo majokofu mawili yaliyonunuliwa katika kituo hicho kwa ajili ya kuhifadhi damu yakabainika kuwa ya matumizi ya nyumbani.

“Ni majokofu kwa ajili ya kufungia nyanya,karoti na parachichi na wataalamu wametuthibitishia kuwa haya sio majokofu ya damu, huyu mzabuni tumemlipa bila kukagua tumeagiza majokofu ya kutunzia damu tumeletewa majokofu ya matunda” Amesema Dkt. Mfaume.

Kufuatia hatua hiyo Dkt. Mfaume ameelekeza mfamasia wa halmashauri kuondolewa kwenye nafasi yake kwa kutoa taarifa ya uongo wakati wa ukaguzi wa vifaa huku akielekeza kuonywa kwa maandishi kwa wajumbe wa timu ya usimamizi wa shughuli za Afya ya Halmashauri (CHMT) ya Msalala.

JAMBO TV
My God!!!
 
Acha kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.........maana keki inatafunwa kisawa sawa
 
Dawa hapo mzabunj na aliyepokea mafriji walipe pesa na washtakiwe kwa uhujumu uchumi.
 
Kwani hamna specifications na pia kwani hamna Wataalamu wa vifaa tiba Hadi mkapokea majokofu ya nyanya?
Ya kuwekea damu bei yake ni x5 ya haya walionunuwa🤣🤣
 
Attachments

  • IMG_7410.jpeg
    IMG_7410.jpeg
    33.5 KB · Views: 3
  • IMG_7409.png
    IMG_7409.png
    99.3 KB · Views: 3
  • IMG_7408.jpeg
    IMG_7408.jpeg
    18.9 KB · Views: 3
Hebu tuongee kwa mapana medical refrigerator na domestic refrigerator zina tofauti gani kwenye ufanyaji kazi? Na kama ulikuwa na medical one ikaharibika utaacha products ziharibike au utazihamishia kwenye domestic?
Hivi umetafakari kweli? Unadhani damu inahifadhiwa hovyo kama maji? Damu inafanyiwa process nyingi na inatenganishwa na kuwa sampuli tofauti na kila sampuli inahifadhiwa kwenye temperature yake. Unapotoa damu siyo kwamba inatumika kama ilivyo.
 
Hapo unaweza kuta mletewaji na mletaji (mzabuni) hawajui ni kitu gani kinatakiwa, pia unaweza kuta zabuni haikueleza aina ya jokofu. Probably uzembe umeanzia mbali.
 
Hebu tuongee kwa mapana medical refrigerator na domestic refrigerator zina tofauti gani kwenye ufanyaji kazi? Na kama ulikuwa na medical one ikaharibika utaacha products ziharibike au utazihamishia kwenye domestic?
Hizi domestic fridge hazina thermostat ambayo inakuwezesha kuset temperature inayotakiwa kwa kuhifadhi sampuli maalumu kawa dawa, reagent na damu kma hivo.
Wangekua smart kidogo wangenunua hata sub zero thermometer zinafungwa hapo damu inakuwa salama ila sio hivyo walivyofanya.
 
Hebu tuongee kwa mapana medical refrigerator na domestic refrigerator zina tofauti gani kwenye ufanyaji kazi? Na kama ulikuwa na medical one ikaharibika utaacha products ziharibike au utazihamishia kwenye domestic?
Medical refrigirator ina temperature control na domestic haina icho kitu so unakua hujui umeweka dam zako ndan mna joto kias gn, na damu ya binadam inatakiw kukaa katk temperature ya 2 to 8 celcius degree
 
Ukipima joto la domestic fridge lina-range ngapi hadi ngapi?
 
Cjajua pia domestic halijakua automatic kukufanya uweze kumonitor temp elewa apo mkuu
Na nikiweka temperature monitoring devices ambazo ni electronic na zinauzwa haiwezi kufaa? Hasa kama imeonekana kutunza joto linalotakuwa
 
Kumonitor na kucontrol ni vitu viwili tofauti, temperature monitoring unaifanya kwa data loggers ambazo ndo hizo electoronic devices au thermometer za kawaida.
Unaweza kumonitor temperature hata kwa fridges za kawaida ambazo ni non controlled fridges.
Ila ukitaka kucontrol jotoridi kwenye friji ambazo sio pharmaceutical lazima utafute thermostat uiinstall hapo kwenye friji kwa ajili ya kuset jotoridi linalotakiwa.
 
Kwani hamna specifications na pia kwani hamna Wataalamu wa vifaa tiba Hadi mkapokea majokofu ya nyanya?
Hii ni changamoto kubwa kwa Hospital nyingi, tena wakati mwingine vifaa vinanunuliwa havina kiwango au haviendani na Technology iliyopo. Shida mwongozo uliopo katika Hospital za serikali, anaehusika na manunuzi ya vifaa tiba ni mfamasia na sio "mtaalamu wa vifaa tiba/Biomedical Engineer" sasa ukiangalia mfamasia hajasomea vifaa tiba.
 
Back
Top Bottom