Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Katika Kata ya Ibadakuli, Manispaa ya Shinyanga, kumetokea sintofahamu kubwa kati ya diwani wa kata hiyo, Msabila Malale, na diwani wa Vitimaalumu, Zuhura Waziri, wakati wa zoezi la kura za maoni za chama cha Mapinduzi (CCM).
Tukio hili lilitokea jana wakati wagombea wa CCM walipokuwa wakichaguliwa kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.
Diwani Msabila alieleza kwamba aliona kasoro wakati karatasi za kura zikiandaliwa hivyo alianza kuhoji usalama wa mfuko wa kura baada ya kura moja ilikung’utwa na kuanguka.
Soma pia: Masasi: Waziri Bashe aagiza diwani wa CCM kutiwa mbaroni kwa tuhuma za kutafuna fedha za wakulima milioni 139
Pia diwani huyo alidokeza kuwa aligundua kwamba msimamizi wa uchaguzi alikuwa akiwasaidia watu wasiojua kusoma na kuandika kupiga kura na hata baada ya kutoa malalamiko lakini diwani Zuhura alijibu kwa maneno makali, akimwambia asiwafundishe jinsi ya kufanya kazi.
Baada ya malumbano ya maneno kuwa makali madiwani hao walianza kutumia nguvu na kuanza kupigana.
Zuhura Waziri alipotafutwa ili kutoa maelezo kuhusu tukio hilo, alikataa kuzungumzia kwa sasa, akisema anajisikia vibaya baada ya kudai kupigwa na diwani Msabila.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anold Makombe, alisema bado hajapata taarifa kamili kuhusu tukio hilo, na atazungumzia baada ya kupata maelezo ya kutosha. Hivi sasa, anaelekea kwenye kikao ofisi za CCM ili kujadili masuala mengine.
Source: IPP Media