John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema ameagiza kuchukuliwa hatua za kisheria walimu watakaobainika kudai malipo kwa wanafunzi akisema elimu ni bure.
Amesema hayo wakati akifungua kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga, leo Alhamisi Machi 3, 2022 chenye lengo la kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
“Kumekuwa na upotoshaji huko mtaani kuwa wazazi wanatakiwa kulipa ada. Napenda kusisitiza kuwa elimu ni bure, hakuna malipo, mwalimu yeyote atakayebainika kuchangisha fedha achukuliwe hatua.
“Tutaendelea kutatua changamoto zilizopo ikiwemo utoro, chakula, upungufu wa walimu n.k,” amesema RC.
Source: Malunde.com