Shinyanga: Mradi wa Machinjio ya kisasa ya ng’ombe yaliyopo katika kata ya Ndembezi, umekwama kukamilika

Shinyanga: Mradi wa Machinjio ya kisasa ya ng’ombe yaliyopo katika kata ya Ndembezi, umekwama kukamilika

RWANDES

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,788
Reaction score
4,401
Naibu waziri Katambi amefanya ziara katika Machinjio ya kisasa ya ng’ombe yaliyopo katika kata ya Ndembezi na kuonesha kutoridhishwa na ujenzi wa machinjio hayo yenye gharama ya Shilingi Bilioni 5.57 ulioanza mwaka 2018 ukitarajiwa kukamilika mwaka 2019 lakini mpaka leo hauoneshi dalili yoyote ya kuanza kufanya kazi, haufunguliwi na hauoneshimatumaini ya kufunguliwa.

“Ujenzi wa mradi huu wa machinjio hauoneshi dalili zozote utaanza kufanya kazi lini. Sikubaliani na hatua ya ujenzi wa mradi huu ambao umetumia fedha nyingi kiasi cha shilingi Bilioni 5.1 mpaka sasa na haujaanza kufanya kazi na kuna mapungufu mengi katika mradi huu, hali inayofanya wananchi wakose kazi na ajira”, amesema Katambi.

Katmbi amesema kutokana na mradi huo wa machinjio kukwawama kuna mambo lazima yachunguzwe ili kuondoa mashaka na hatua za kisheria "Lazima hatua zichukuliwe ili tujiridhishe kama fedha zimetumika kiha tujue,sasa ni wakati wa kuchukua hatua".

“Haiwezekani viwanda vya Shinyanga kila vinapoanzishwa vinakwama, kile kiwanda cha Old Shinyanga kilishakwama. Najua viongozi wengi wakiwemo Mawaziri wamewahi kufika hapa na kuahidiwa kuwa kiwanda kitafunguliwa punde lakinihakifunguliwi.

Maelezo ni haya haya hatua hazikuchuliwa, Mimi sitakubali kiwanda kukwama,hatuwezi kuwa tunaimba kila siku, hatua hazichukuliwi, jambo hili nalichukua nitalipeleka katika mamlaka zinazohusika na ni lazima hatua zichukuliwe kwa yeyote aliyesababisha mradi huu ukwame.

Ni lazima tujue mbivu na mbichi kama mradi huu unafunguliwa au la. Na kama haufunguliwi tujue fedhazimeenda wapi”,ameongeza Katambi.

Hata hivyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Mhe. David Nkulila amesema manispaa ya Shinyangakupitia kamati ya fedha imeagiza kuitwa na kuhojiwakwa Wakuu wa Idara wa Manispaa ya Shinyangaakiwemo aliyekuwa Afisa Mifugo waManispaa, Afisa Mipango, Mhandisi, AfisaManunuzi, Mhandisi Mshauri, Contractor wa mradi HomeAfrica Investment ili waeleze kuhusu sababu za kukwama kwa mradi huo na Mkurugenzi wa Manispaa achukue hatua za kisheria.
 
Hapo Katambi ndiyo anaenda kujichimbia kaburi kabisaaaa!

Meya wa CCM unaenda kuvutananae umesahau walivyo kubeba kwenye box la kura feki?
Wabunge wa Bahati Nasibu. Huyu hata angepambana na mmiliki baa ya Bakulutu pale Kambarage asingepata hata 30%.
 
Wabunge wa Bahati Nasibu. Huyu hata angepambana na mmiliki baa ya Bakulutu pale Kambarage asingepata hata 30%.
Ana laana ya Mzee Mbowe

Jinsi alivyo lelewa vizuri kisiasa na Mbowe na alivyokuja kumgeuka na kuikejeli Chadema na Uongozi mzima

Kweli malipo hapa hapa duniani leo aliyekuwa akimtukuza yupo wapi?
 
Hii miradi inayoanzishwa kwa maagizo ya kisiasa itakufa yote, na hata daraja la kigogo-busisi laweza kusimama na kufa muda wowote.
 
CCM ngumu sana kuwasimamia, wao huwa wanawaza mbinu mpya za kuiba tu.
 
Hivi si billion 1 ndo sawa na million 1000 au? Ka ndo hvyo inamaana huo mradi wa apa ndembez umetumia million 5100 dah! Tanzawizi n noooma... ! Afu mbaya Zaid mradi haujaisha!
 
Back
Top Bottom