Shinyanga: Mume amuua Mkewe akimtuhumu kutumia ARV kwa siri

Shinyanga: Mume amuua Mkewe akimtuhumu kutumia ARV kwa siri

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia, Peter Elias (29) mkazi wa Ndembezi mkoani humo kwa tuhuma za kumuua mkewe, Pili Luhende akimtuhumu kutumia dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARV) kwa siri.

Akizungumza Ijumaa Mei 7, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Mei 3, 2021 katika mtaa wa Dome kata ya Ndembezi.

Amesema mtuhumiwa alimpiga Pili maeneo mbalimbali mwilini na alipobaini amefariki dunia, aliuchukua mwili wake na kwenda kuutupa maeneo ya daraja la Mwagala.

"Baada ya taarifa hiyo mtuhumiwa tulimkamata na kumhoji ambapo jana alionyesha alipoutelekeza mwili wa marehemu maeneo ya Mwagala darajani.”

“Baada ya kuhojiwa alibainisha kuwa alimpiga kwa ngumi chanzo kikiwa ni mtuhumiwa kumbaini mkewe anatumia dawa ARV kwa kificho jambo lililomkasirisha na pia alisema walikuwa na ugomvi wa mara kwa mara,” amesema kamanda huyo.

Amesema mwili ulikutwa ukiwa umeharibika na ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Chanzo: Mwananchi
 
Kama alitumia kwa siri maana yake kuna namna ambayo inatia shaka!

Kwanini hakustuka na kumshirikisha mwenzie waende hospitali.

Sijui alikosa ushauri!

Yazidi kutuepuka mabaya , Eeeh Mwenyezi Mungu uzidi kutuhurumia na kutuepeshia mbali mabaya!
 
Kwani nimetaja mtu Leo?? Nimesema sijataja Wasukuma
Nakumind kinoma! Umeishi jamii za kisukuma unawajua vzr...lini ulisikia hatuzijui arv?kwamba mwendazake alikua anahusudu wamama weupe wenye mizigo(in sheikh kipoozeo's voic) basi imekuwa wote?hapana hili halikubaliki...nakukumbush tena wewe ni verified member...
 
Sijawahi kujua hili, umejuaje?
 
Back
Top Bottom