Shinyanga: Mume aua mke wake kwa Panga akimtuhumu kusaliti Ndoa yao

Shinyanga: Mume aua mke wake kwa Panga akimtuhumu kusaliti Ndoa yao

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mwanaume anayejulikana kwa jina la Heneriko John (53) mkazi wa Manispaa ya Shinyanga, amedaiwa kumuuwa mke wake Regina Jiyenze (45) kwa kumkata mapanga kichwani na mabegani, kisha kujisalimisha kwa Jeshi la Polisi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, amesema tukio hilo limetokea Oktoba 5, saa tatu asubuhi katika Mtaa wa Mbulu Kata ya Mhongolo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Kyando amesema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, ambapo mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa sio mwaminifu kwenye ndoa yao, kitendo ambacho kilimfanya mtuhumiwa kujichukulia sheria mkononi na kumkata mapanga na kusababisha mauaji.

“Katika eneo la tukio tumeokota panga lenye damu likiwa umbali wa mita 20 kutoka katika eneo la tukio lilipotendeka, mtuhumiwa tunamshikilia mara baada ya kujisalimisha mwenyewe, na tutamfikisha mahakamani baada ya upelelezi kukamilika,” amesema Kyando.

“Mtuhumiwa alitumia mbinu ya kumvizia mke wake na kumkata mapanga wakati akiwa nyumbani kwa balozi Manungu Bundala, alipofika kwa ajili ya kushitaki kutishiwa kuuawa na mume wake, ndipo alipokatwa mapanga sehemu za kichwani na mabegani na kufariki dunia,” amesema.

Aidha kamanda alitoa wito kwa wananchi kujiepusha na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi kisa wivu wa mapenzi, kwani kitendo hicho hakifai na kinaonekana kimekuwa sugu.

Ametoa ushauri kwa wapenzi au wanandoa, kuwa wakiona mwenzake sio mwaminifu kwenye mahusiano ni bora waachane kuliko kuchukua hatua mbaya kama hiyo.

Chanzo: Mwananchi
 
Watu wa mikoani wapo serious sana

Kuna yule boya alimpiga faini mtu kisa uroda yaani ni matakataka

Sijui mavyakula wanayokula yanawapunguzia akili kisha yanawaongezea nyege
 
Eti atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika. Mtuhumiwa kaua mbele ya balozi, akajipeleka mwenyewe Polisi kuwaambia nimeua, sasa upelelezi gani wanautaka?

Maiti ipo, panga lipo, balozi yupo, mtuhumiwa yupo!

Polisi bhana!
 
Eti atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika. Mtuhumiwa kaua mbele ya balozi, akajipeleka mwenyewe Polisi kuwaambia nimeua, sasa upelelezi gani wanautaka?
Maiti ipo, panga lipo, balozi yupo, mtuhumiwa yupo!
Polisi bhana!
Kesi ni process mkuu lazima watafutwe mashahidi zaidi ya mmoja aliyeshuhudia tukioa sio kuambiwa, Polisi walienda baada ya mtuhumiwa kujipeleka so lazima wajiridhishe watachoiambia mahakama, na ushahidi wao usiache shaka.
 
Kesi ni process mkuu lazima watafutwe mashahidi zaidi ya mmoja aliyeshuhudia tukioa sio kuambiwa, Polisi walienda baada ya mtuhumiwa kujipeleka so lazima wajiridhishe watachoiambia mahakama, na ushahidi wao usiache shaka
Na ni hizo process zilizoifanya mfumo wetu wa haki kuwa wa hovyo kabisa.

Kesi kama hii utajaona inachukuwa miaka kuisha. Kesi hii haikupaswa kudumu mahakamani hata kwa mwezi moja, kuondoa mrundikano wa vyesi mahakamani.
 
Kuua mwenzio kwa mapanga aisee, yaani unamkata kama mti aisee kuna watu wana roho ngumu, adhabu ya kunyonhwa ingekuwa ina sainiwa tu mtu kama huyu anyongwe tu
 
Na ni hizo process zilizoifanya mfumo wetu wa haki kuwa wa hovyo kabisa.

Kesi kama hii utajaona inachukuwa miaka kuisha. Kesi hii haikupaswa kudumu mahakamani hata kwa mwezi moja, kuondoa mrundikano wa vyesi mahakamani .
Ukiua kwa kukusudia kunamambo mengi lazima yachunguzwe ikiwemo afya ya akili, kujua hasa kiini cha tukio anyway mi sio Mwanasheria ila hata kesi za zake huwa haziamuliwi mapema inaweza kuchukua hata mwaka kuamuliwa
 
Ukiua kwa kukusudia kunamambo mengi lazima yachunguzwe ikiwemo afya ya akili, kujua hasa kiini cha tukio anyway mi sio Mwanasheria ila hata kesi za zake huwa haziamuliwi mapema inaweza kuchukua hata mwaka kuamuliwa
Nisaidie kitu. Kuchelewesha kuna faida gani?! Au mafungu mpaka yaidhinishwe! Ahahahahaa [emoji23][emoji1787][emoji102]
 
Nisaidie kitu. Kuchelewesha kuna faida gani? Au mafungu mpaka yaidhinishwe! Ahahahahaa [emoji23][emoji1787][emoji102]
Ugumu wa kesi ni mashahidi wengi wameona ila watakaokuwa tayari kutoa ushahidi ndio mtihani unaanzia hapo hasa ukizingatia hii kesi itasomwa mahakama za kawaida wakati upelelezi unaendea then baadae inahamishiwa Mahakama kuu ukute hiyo mahakama kuu ipo mwanza nani ataacha kazi zake asafiri kwa garama zake na ajitegemee malazi?

Siku ya tukio watu hujaa ila wakiona polisi walioshuhudia tukio likitendeka wanaingia mitini
 
Back
Top Bottom